Na Mwandishi Maalum, New York 
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, jana alhamisi amezindua rasmi mwongo wa Nishati Endelevu kwa wote (SE4ALL) wakati wa mkutano unaohudhuriwa na wajumbe zaidi wa 1,000 wakiwamo zaidi ya mawaziri 20 wa Nishati 20 wafanyabishara, mashirika ya kimataifa yakiwamo ya fedha na Asasi zisizokuwa za kiserikali.
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huu ulioanza Juni 4 na utamalizika Juni 6, unaongozwa na Waziri wa Nishati na Madini Professor Sospeter Muhongo ( Mb) ambaye pamoja na kuhudhuria na kuchangia mijadala mbalimbali leo Ijumaa  June 6, atazungumza katika mkutano wa mawaziri kuhusu nafasi ya Nishati katika Ajenda za Maendeleo Endelevu baada ya 2015. 
Akizindua mwongo huo Ban ki Moon, pamoja na mambo mengine alieleza kuwa licha ya kuwa pamoja suala la Nishati ni suala la kidunia, lakini katika maeneo mengi ni suala linalomhusu mwanamke zaidi. 
“ Ni suala linalomhusu mwanamke zaidi, linaweza kumaanisha tofauti kati ya usalama na hofu, uhuru na utumwa , hata uhai na kifo. Dunia lazima ije pamoja kumaliza umaskini wa nishati na kuhakikisha watu maskini wanaweza kuhimili maisha yao na kustawi kiuchumi” akasema Katibu Mkuu. 
Akaongeza kuwa mpango wa nishati endelevu kwa wote zimeanza kuzaa matunda na kwamba ahadi za mabilioni ya dola zilizoahidiwa zimetolewa, huku nchi zinazoendelea zaidi ya 80 zimejiunga na mpango huo. 
 Pamoja na Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa kuzungumza wakati wa uzinduzi wa mwongo huo, wengine waliopata nafasi ya kuzungumza ni pamoja na Rais wa Iceland, Olafur Ragnar Grimsson, Bw. John Ashe,Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Rais wa Banki ya Dunia Jim Yong Kim ( kupitia video) . 
 Mkutano huu utafanya tathmini ya matokeo ahadi za mabilioni ya dola kuhusu upatiakani wa nishati, ufanisi wake na nishati mbadala zilizoahidiwa wafanyabiashara, wawekezaji na watu wengine walizotoa wakati wa Mkutano wa Maendeleo Endelevu ( Rio+20) uliofanyika mwaka 2012. 
Aidha unatarajiwa kuhamasisha upatikanaji wa raslimali fedha, uwezeshaji na mipango ya kufikia malengo ya nishati endelevu kwa wote.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban Ki  Moon, akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Mwongo wa Nishati Endelevu kwa  Wote (2014-2024),  uzinduzi huo umefanyika wakati wa Mkutano wa Kwanza wa  Mwaka kuhusu Nishati  Endelevu kwa Wote  ( SE4ALL)unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 1000.  Waziri wa Nishati na Madini,  Mhe. Profesa Sospeter Muhongo ( Mb) anaongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huu. 
 Wajumbe wanaohudhuria  Mkutano wa Nishati Endelevu kwa Wote wakiwa katika picha ya  pamoja na  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. John Ashe mara baada ya uzinduzi wa Mwongo wa Nishati kwa wote. Mhe.  Waziri  Muhongo anaonekana nyuma ya Katibu Mkuu
 Mhe. Waziri wa Nishati na Madini  Profesa Muhongo akiwa na Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi muda mfupi  kabla ya uzinduzi wa Mwongo wa Nishati Endelevu kwa Wote.  Walioketi nyuma ni wasaizidi wa  Waziri.
Sehemu wa  washiriki wa  mkutano wa Nishati Endelevu  kwa wote wakifuatilia uzinduzi wa Mwongo wa  Nishati kwa wote .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2014

    Nishati kwa wote ni ujumbe muafaka kwetu sisi watanzania.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2014

    Tuwe na mkakati wa kusitisha kuchora kuchoma makaa na kukata miti. Ama sivyo ni shati ya wa kubwa tu. Hii gesi twaisikia tu iko wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...