Malkia wa Swaziland Mheshimwa Nomsa Matsebula akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Ndugu Nurdin Babu mara baada ya helikopta iliyomchukua kutua kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Nyamisati huko wilayani Rufiji ambako alikwenda kutembelea Shule ya Wamanakayama inayomilikiwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA. Tarehe 2.7.2014. Kulia ni Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete.

 Mke wa Mfalme Mswati III wa Swaziland Malkia Nomsa Matsebula akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wamanakayama Dkt. Ramadhan Dau mara baada ya mgeni huyo kuwasili huko Nyamisati
 Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula akiwa amefuatana na mwenyeji wa Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Nyamisati waliofika kumlaki mara baada ya helikopta iliyomleta kutua kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Nyamisati
 alkia wa Swaziland Nomsa Matsebula akionyeshwa namna wanavyotumia I-pad katika baadhi ya masomo yao hapo shuleni Wamanakayama na mwanafuzi Rehema Shao aneyesoma kidato cha pili huko mwanafunzi Asia Idd (kushoto) akisubiri zamu yake.
 Mwanafunzi Assia Idd akimwonyesha Malkia Matsebula kutoka Swaziland namna ya kutumia i-pad kwenye masomo ya sayansi na hesabu wakati Malkia huyo alipotembele Shule ya Sekondari ya Wamanakayama inayomilikiwa na Taasisi ya WAMA inayoongozwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...