Waziri wa wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh.Eng Christopher Chiza amewataka wanunuzi wa tumbaku kuja na mikakati mipya ili kuwanufaisha na kuimarisha soko la wakulima wa tumbaku. 
Mhe. Chiza ameyasema hayo leo ofsini kwake alipokutana na Meneja mkuu wa kampuni ya ununuzi wa tumbaku kutoka kampuni ya JTI. 
 Pamoja na mambo mengine waziri amewataka wafanya biashara hao kuaanda mikataba kwa lugha ya Kiswahili na kingereza ili kuwafanya wakulima waelewe masharti na manufaa ambayo yanaweza kupatikana katika mikataba hiyo 
Akiongea na meneja mkuu wa Kampuni hiyo Bwana Robert Glenn amewataka kuleta mabadiliko chanya kuanzia kwenye hatua ya ulimaji hadi kwenye soko la zao la tumbaku 
Aidha naye Bwana Robert amesema kuwa Kampuni yake imejipanga kupeleka huduma za ugani kwa wakulima wa tumbaku ili kuongeza ushindani na wafanyabiashara wengine wa ndani na nje.

Waziri wa  wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh.Eng Christopher Chiza akiongea na  meneja mkuu wa Kampuni  ya JTI Bwana Robert Glenn kuhusu ununuzi wa zao la tumbaku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...