Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Bi. Hawa Ghasia ameridhishwa na tathimini ya mkutano wa mashauriaono wa awamu ya kwanza wa Mradi wa Mabasi yaendeyo Haraka (DART) uliofanyika hivi karibuni na wa kampuni ya Simon Group inayomiliki mabasi ya UDA na wamiliki wa usafirishaji jijini Dar es Salaa( Daladala) kuungana kwani italeta maendeleo katika sekta ya usafiri jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam hivi karibuni kuhusu maendeleo ya   ya sekta ya usafiri pamoja na majadiliano yanayoendelea kufanyika wakati huu wa kuelekea katika mfumo mpya wa Mabasi yaendeyo Haraka,Waziri Ghasia aliunga mkono jitihada zote zinazofanywa na wadau katika sekta ya usafiri.

“Kwa jinsi ambavyo mfumo unatakiwa uendeshwe na kwa jinsi  zabuni zitakapo tangazwa bila kua na umoja itakuwa ni vigumu watanzania kupata kazi,”alisema na kuunga mkono makubaliano ambayo yameshafikiwa baana ya pande husika.

Bi. Ghasia alisema uzoefu unaonyesha kuwa watazania wamezoea kufanya kazi mtu mmoja mmoja hivyo basi wakati  umefika wakati kuwa na kampuni moja itakayokuwa na nguvu katika sekta ya usafirishaji.“Imani walioijenga kwa kuungana italeta tija kubwa kiuchumi katika sekta ya usafiri katika  jiji la Dar es Salaam na wengine nao wataiga,” alisema Ghasia.

Alisema  kuwa mfumo  mpya utakaokuwa unatumika katika uendeshaji utakuwa wa kisasa zaidi na kwa mfumo wetu wa kuchukua nauli ndani ya daladala hautakuepo tena hivyo ni lazima kuwa kitu kimoja.

“Mimi ni ningefurahi sana kama huu mfumo ungeshikiliwa na watanzania kuliko wageni,” Waziri Ghasia alisisitiza, na kuongeza kuwa wakati umefika kwa watanzania wabadilike na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Bi. Ghasia alisema anaamini wawekezaji wa ndani wanauelewa mzuri na mfumo huu mpya hasa kutokana na kushirikishwa toka mwanzo wa mradi hadi kufikia sasa kutokana na kujifunza mambo kadha wa kadha nje ya nchi.“ Ninashukuru tumekuwa na wamiliki wa usafiri toka zoezi hili linaanza, DARCOBOA tumeenda nao mapaka Bogota nchini Colombia na wameona namna mfumo unavyofanya kazi” aliongeza Waziri Ghasia.

Alisema kuungana kwao ni ishara na namna walivyojifunza nchini Colombia jinsi wenzao walivyohama kutoka katika mfumo kama tulionao sisi na kuingia katika mfumo mpya wa mabasi yaendayo haraka.

“Wawekezaji wetu waliona namna mfumo ulivyomzuri na rahisi katika jiji lile hivyo ni somo tosha kwa wamiliki wetu wa hapa nchini, nashukuru wameliona hilo,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...