WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe amekutana na Mwanaharakati wa Kimataifa wa haki za wanawake na watoto, Graca Machel na kujadili masuala mbalimbali ya haki za wanawake na watoto katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.

Katika mazungumzo yao, Waziri Chikawe alimwambia mke huyo wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, juhudi zake za kuingiza katika Katiba Mpya kifungu cha kuzuia mtoto wa chini ya miaka 18 asioe wala asiolewe.

Hata hivyo, Mama Machel kwa upande wake alimshukuru Waziri Chikawe kwa maoni yake na kusema kuwa ni muhimu kwa wadau wote wa haki za watoto wakashinikiza wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na watunga sheria wote wahakikishe kipengele hicho kinaingia ndani ya Katiba. Mama Machel yupo nchini kuhudhuria mkutano wa ufunguzi wa Kampeni ya Kitaifa ya kutokomeza ndoa za utotoni.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (Kushoto) akizungumza na Mwanaharakati wa Kimataifa wa haki za wanawake na watoto, Graca Machel katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo. Waziri Chikawe alimueleza Mama Machel, juhudi zake za kuingiza katika Katiba Mpya kifungu cha kuzuia mtoto wa chini ya miaka 18 asioe wala asiolewe.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akiagana na Mwanaharakati wa Kimataifa wa haki za wanawake na watoto, Graca Machel baada ya kikao chao kifupi kilichofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo. Waziri Chikawe alimueleza Mama Machel, juhudi zake za kuingiza katika Katiba Mpya kifungu cha kuzuia mtoto wa chini ya miaka 18 asioe wala asiolewe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

 1. Jamanii usiniangalie mimi hivyo naona aibu....

  Tehe tehe tehe tehe tehe.... karibu tena Tanzania, nami ni jirani yako hapo Nachingwea njoo uitembelee nyumba MLIOISHI wakati wa vuguvugu la uhuru wa Nchumbiji...

  Ntakutembeza UFURAHI...

  ReplyDelete
 2. nimeipenda hiyo comment ya kwanza...

  ReplyDelete
 3. Mama anajua kujimaintain, ametoka kuomboleza mumewe anaendelea na kazi ya kuhamasisha ulimwengu katika maendeleo na haki za wakina mama na watoto.

  ReplyDelete

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...