Mama wa Mitindo Asia Idarous-Khamsin akimuandalia vazi la khanga mchekeshaji na MC  maarufu nchini Zipompapompa ambaye ni mmoja wa wasanii mashuhuri wataonogesha tamasha kubwa la aina yake la SIKU YA MSANII Jumamosi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam. Msikilize Zipompapomba hapo akitoa yake chini...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hahahahaha ungejua huku hao wazungu unaowatolea mfano kama ndio wanakesha ktk hizo simu wala usingesema.....nilichokigundua ni kwamba kuna ile kukariri kwamba wazungu ni smart kumbe hata hilo suala la kutokupiga mswaki au kunawa uso sio la routine....tena juzi tu wala siongopi classmate wangu tena anatokea Taifa kubwa lenye nguvu za kila aina kaja darasani bila ya kunawa uso na matongotongo kibao masikini huwezi amini, haya hiyo haitoshi suala la kuoga mimi nagombana na shemeji yenu kila siku yaani mpaka nafikia kumwambia usipooga hupati dawa.....kwahiyo msidhani kila king'aacho ni dhahabu hakuna kitu , kwaleo tuishie hapa nina uzoefu wa miaka kumi ya kuishi mashariki na magharibi ya Ulaya.....ovyoo tu...

    ReplyDelete
  2. Duh! Khatari, lakini kuna kaukweli hapa

    ReplyDelete
  3. Hahhahah...eti bwana wa maana,in a unaweza ukawa una bwana sema sio wa maana, mademu wa kibongo..mie hoi

    ReplyDelete
  4. Mimi nina miaka mingi na wanae nipo huku ulaya.Ninapata uchungu sana hii ni kashfa kubwa, na inanitia huzuni sana ninaposikia watu wakiiponda bongo na wabongo kuwa tupo nyuma ukilinganisha na ulaya.Karibuni njooni mjionee wenyewe huo mnaouita ustaarabu. Utumwa na ukoloni umetuacha na makovu mengi.

    ReplyDelete
  5. Dada yangu Zimpompapompa laiti ungelijua usingesema! Ni bora hao wanaocheza na simu, hivi unajua jamaa zetu hawa kuoga kwao ni ishuu? Unamkuta anaingia chooni anamaliza haja zake hata mikono hanawi yaani tatizo sio bongo tu, ni kila sehemu . Labda Arabuni naweza sema wako wasafi sana sababu na mila na desturi zao za kutawadha kila wanapotaka kwenda Ibadani. Ila huku ughaibuniii sio kabisa. mambo ya toilet paper!! huwi msafi ng'oo

    ReplyDelete
  6. Hivi wabongo mmkoje mbona mnashindwa kusoma vitu ambavyo ni 'very simple' tu. Dada Zimpompapompa ujumbe wake kwa akina dada ni kujitambua na wasitekwe na vitu hivi kama simu. Na aliyozungumza yote ndio yanayotendeka. Sasa nyinyi mnaacha kuchangia mada ujumbe badala yake mnamjadili yeye na kujitia mmmekaa ulaya miaka mingi...binafsi nimeishi US mwaka wa 35 sasa na sipigi kelele?

    Eleweni na jadili mada /ujumbe ujumbe jama badala ya kujatapia mika uliishi ughaibuni.

    ReplyDelete
  7. Mjumbe hapo juu unasema umekaa nnje miaka 35 hupigi
    Kelele?una manana gani wakati umepiga kelele tayari?
    Mtu ambae hapigi kelele haandiki chochote.

    ReplyDelete
  8. Dada yetu ! usilolijua litakusumbua kama ungewajua wazungu teen wao ndio simu zimewatia wazimu hadi wanapelekwa Therapie za kutulizwa akili dada njoo ulaya uone wazungu mtu kwa wiki anakoga mara moja

    ReplyDelete
  9. Mdau uliosema eleweni na jadili mada umeongea kitu cha kweli haya ndio matatizo yetu sie Huyu Mie naweza kumuita Mama, yeye akaongelea jambo la kweli na yeye akaongelea Dada zetu kwahiyo msiwe Mnachukia pimeni ukweli na muiweke sawa na akija kuongelea wa kiume pia tutachukulia na kujiweka pale tulipokosa Kuwa sawa, Hilo la wazungu fanyeni Kama mnaliweka pembeni yeye Kasema tu waliotengeneza simu ila kwake anaongelea kitu alichokiona kwa macho yake kwa wakina dada bongo ili ifanyiwe kazi na wakina dada wa bongo hakufanya kwa chuki ni busara siku hizi vijana tunakuwa wabishanaji ndio tatizo la sijui Ulaya wabaya au wazuri sio mada aliongelea. Mz

    ReplyDelete
  10. Bwana mwamerika tunakuomba radhi.Lakini ni yale yale hata kwako.Yaani wabongo twashindwa hata kusoma kitu very simple. Banaa sisi wabongo, umesahau?.Umekaa Amerika miaka mingi sana, mashaa Allah, Mungu akuzidishie.Miye ninaposema nimekaa ulaya miaka mingi, mwaka huu ni wa arubaini na sita na watoto wake.

    ReplyDelete
  11. Anachokisema huyu bibie ni sawa kabisa kwani watoto wanaukumbatia ujinga tu hawafati maadili yetu. Je kushinda na simu siku nzima ndio maendeleo? Hata hao wazungu wanatumia simu kwa wakati na sababu maalum. Sehemu nyingi zinapiga marufuku utumiaji wa simu haswa makazini hospitali mashuleni nk. Hao wanaotumia simu wakati wote ni wafanya biashara ambao kipato chao kinatokana na mawasiliano ya simu . Wale wasiokua na kazi ndio wanaozungumziwa hapa . Watafute kazi. Acheni kuendekeza watoto wenu.

    ReplyDelete
  12. hahahahahahahah mpe huyo mwamerika...

    ReplyDelete
  13. Na kweli mdau wa Amerika wabongo tuna matatizo ya ulewa wa simple thing.

    Inanikumbusha zamani kwenye mtihani wa somo la kishwahili ulikuwa unapewa swali linasema soma taarifa ifuatayo (ambayo ni kama page moja nzima hivi juu ya mada fulani) kisha unaambiwa jibu maswali yafuatayo (kama kumi hivi). Yote ile ilikuwa ni kupima uwezo wa utindio wa uelewa wa mwanafunzi.

    Na kwenye mtihani wa english kulikuwa na Composition kwa mtindo huo huo.

    Sasa hapa badala ya kujikita kwenye mada watu wameokota kajineno ka 'mzungu' tu ndicho walichoona kwenye ujumbe. Taabu kubwa walahi.

    Na ndio maana viongozi wetu wa leo hata hawajui kwa nini Tanzania bado masikini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...