Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Ndugu Li Yuanchao wakati walipokutana kwenye Sherehe ya kutimiza Miaka 50 ya Uhusiano wa Kidiplomasia baina ya Tanzania na China. Sherehe hizo zilizoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini China na kufanyika jijini Beijing leo
 Makamu wa Rais wa China Ndugu Li Yuanchao akigonganisha  glasi ikiwa ni ishara ya kusherehekea kutimiza miaka 50 ya ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China. Sherehe hizo zilifanyika jijini Beijing 
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akigonganisha glasi na  Mama Salma wakisherehekea kutimiza miaka 50 ya ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na China.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Bernard Membe wakisherehekea kutimiza miaka 50 ya Ushirikiano wa Kidiplomasia baina ya Tanzania na Cina kwa kugonganisha glasi zao huku Mama Salma na Makamu wa Rais wa China Ndugu Li Yuanchao (aliyesimama kulia)  wakishuhudia. Sherehe hizo zilifanyika Beijing nchini China leo. PICHA NA JOHN  LUKUWI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Wachina tuliwasaidia sana ndio maana hawabanduki kwa tanzania

    ReplyDelete
  2. Wachina walitusaidia sana mdau hapo juu kama huji. Toka enzi za Mao Zhe Tung. Wamejenga TAZARA miaka hiyo!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ndio hujui historia ilivyo , so kaa kimya au uliza ufahamishwe bwana mdogo

      Delete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...