THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MAZISHI YA RAIS SATA WA ZAMBIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata Ikulu mjini Lusaka Zambia jana Novemba 11,2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal wa kwanza (kushoto) akiwa na Rais Mstaafu wa Zambia Mhe. Rupia Banda, Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, Rais wa Msumbiji Mhe. Ermando Guebuza na Kaimu Rais wa Zambia Dkt. Guy Scott kwenye Misa Maalum ya kuaga mwili wa Rais Michael Sata iliyofanyika jana Novemba 11,2014 kwenye Uwanja wa Taifa mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha Tawala cha PF Mhe. A.B. Chikwanda kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa wakati mazishi ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata yaliyofanyika jana Novemba 11,2014 kwenye uwanja wa Taifa mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji Rais mstaafu wa kwanza Zambia Dkt. Keneth Kaunda mara baada ya kumalizika maziko ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika jana Novemba 11,2014 mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji Rais mstaafu wa Zambia Mhe. Ruphia Banda baada ya kumalizika mazishi ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika jana Novemba 11,2014. katikati Rais mstaafu wa kwanza wa Zambia Dkt. Keneth Kaunda. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisaini kitabu cha maombolezo ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika jana Novemba 11,2014. (Picha na OMR)