Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Dada Shamsa Danga, malalamiko ya wasanii wetu yanajulikana na kila mtu. Kulaumu kitu kwao ni rahisi sana, lakini mtu ukitaka kusema ule ukweli kutoka moyoni mwako utapata jibu.
    Wasanii wa filamu kwa kuuziwa kazi zao kwa bei ya chini siyo tatizo. Je, kazi zao wanazozifanya wanaziona zinastahili kuuzwa bei kubwa? Je, ni gharama kubwa kiasi gani inawagharimu katika kuzitengeneza filamu zao hizo? Je, zinakiwango na bei wanazozidai wao?
    Hata hivyo, sitaki kuwakatisha tamaa ndugu zangu hawa. Mimi nataka kuwakaribisha katika studio ya kampuni yangu ya MSOL AB ambayo kampuni hii itakurekodia kazi zako zote na kama utahitaji Director itakupa, baada ya kurekodi kazi yako itakusambazia kazi yako katika mitandao ya dunia iTunes, sportify, amazon, youtube na zingine ambazo kampuni inamakubaliano nayo.
    Tatizo lililopo kwa wasanii wetu hawasomi mitandao kama hii na hata hii ya Michuzi. Wamejikita zaidi katika kusoma mitandao ya udaku. Dada Shamsa, waamshe na uwaambie kuwa wanapitwa na fursa adimu kama hii kwa kukalia kusoma habari za udaku tu. Waambie waingie katika tovuti ya www.msolab.seLakini usihangae kwa kuona kuwa hakuna atakayetembelea na ku-like MSOL.

    Peters Mhoja - Sweden

    ReplyDelete
  2. Bongo Movie achene kupiga mayowe, fanyeni kazi zenye ubora mkubwa na pia script zinazozingatia maadili kuwa familia inayojumuisha rika, jinsia, ukwe inaweza kuangalia filamu zenu kwa pamoja.

    Mkizingatia hayo basi customers watakuwa hawana tatizo kununua kazi iliyo bora inayozingatia angalizo hapo juu kwa bei nzuri hata nyie mkafurahia.

    Lakini mkifanya filamu zisizo na viwango halafu watu wanaogopa kuingalia kwa pamoja kama familia ktk sebule zao basi mtandelea kupiga mayowe sana na wala serikali haiwezi kupanga bei eti filamu iuzwe kiasi Fulani.

    Kazi kwenu na inaanza na nyinyi wenyewe kufanya vitu vya uhakika hata Babu akanunua kazi zetu ili aangalie na wajukuu zake pamoja na wakwe zake bila kupata na presha ya mambo ya ajabu ajabu kuoneshwa kwenye filamu zenu huku pia ikiwa haina hata mtiririko mzuri wala hadithi na ma-actor wanao zifanyia haki nafasi zao ktk filamu husika.

    Mdau
    Mwoga-kuangalia filamu za Bongo na familia yake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...