Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi wa katika mkutano uliofanyika mchana huu kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Wizara hiyo,zilizopo kwenye Mtaa wa Samora,Jijini Dar es salaam.
Waziri Muhongo ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo,kufuatia shinikizo la muda mrefu la kumtaka afanye hivyo au awajibishwe, kufuatia mapendekezo ya Bunge lililopita, lililoagiza serikali kuchukua hatua dhidi yake na wengine kadhaa kufuatia kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.

Waziri Muhongo akikazia kujiuzulu kwake huko amesema kuwa yeye sio mla rushwa bali ni mchapa kazi tu na akilizungumzia swala la akaunti ya Tegeta Escrow ambalo ndilo lililopelekea kujiuzulu kwake huko,Waziri Muhongo amesema kuwa sakata hilo lilitawaliwa na mambo makuu manne ambayo aliyataja kuwa ni Mvutano wa kibiashara, Mvutano wa kisiasa, Mvutano wa uongozi na madaraka pamoja na Ubinafsi.
Hivyo kasema ameamua kujiuzulu ili kuiachia Serikali na Bunge kusitisha malumbano ya sakata la Escrow, akidai inaonekana yeye ndiyo tatizo.Picha/habari na Othman Michuzi.
Sehemu ya Waandishi wa kutoka vyombo mbali mbali vya habari wakifatilia kwa makini taarifa ya Waziri Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akisisitiza jambo wakati akilizungumzia swala la Akaunti ya Tegeta Escrow ambalo ndilo lililopelekea kujiuzulu kwake huko,mchana wa leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

 1. Watz tunapenda longolongo. Tutamkumkumbuka Prof. Muhongo. Kwa jinsi tunavyoshabikia bila kuwa analytical kwa kiasi nchi itapoteza hazina ya commited leaders kwa kashfa eti kuwajibika kwa ajili shirika liko chini yako,This is full B.S. Hizi sheria hazina tija kwa karne hii. Inatakiwa wawajibishwe wale wezi.

  ReplyDelete
 2. Makubwa haya
  Ila tafadhali ankal ama mdau yeyote ajuaye zaidi matatizo haya ya Tageta Escow atueleze sisi tusiojua nini hasa mwanzo wa tatizo hili, na wapi naweza kujisomea kwa kina janga hili.

  ReplyDelete
 3. Basi Mungu awe pamoja nawe, tunashukuru kwa kuifikisha Tanzania hapa tulipo kwa masuala ya maendeleo ya umeme. Daima palipo na ukweli uwongo huonekana, hivyo tusubiri tu ukweli utajulikana mbeleni. Mungu ibariki Tanzania yetu

  ReplyDelete
 4. Pia arudishe pesa za escrow, mtu amefanya ufisadi alafu munamuacha tu hivi hivi

  ReplyDelete
  Replies
  1. Do u have proof????kama huna facts,kaa kimya na ignorance yako. Innocent until proven guilty!!!

   Delete
  2. If shit happens under your guard... You are responsible.. sasa semeni mtakavyo... The dude is responsible in one way or another.

   Awajibishwe!!!

   Delete
 5. jamaa yuko vizuri.watakua wamemtoa kafara but hiki ni kichwa haswa ambacho kitawagharimu sana watz siku za usoni...vita ya gesi na oil hii imemcost uwaziri ...
  mdau wa UK

  ReplyDelete
 6. mmh huyu Prof. hakuna kitu. Sasa mbona umebagua tu kuwa eti kama kuna mtanzania alimpatia rushwa. Kwanini asiseme kama kuna mtu yeyote aliyewahi kumpa rushwa na sio watanzania tu?

  ReplyDelete
 7. Laana ya mafuta na gesi inapiga hodi! KARIBU!!

  ReplyDelete
 8. Sio mla rushwa Huyo lkn mambo ya oil ma gas . Matajiri wanataka wawe agents

  ReplyDelete
 9. Pro Muhuongo ulisema huachii ngazi sasa imekuwaje? Ulisema ukiachiswa ardhi ya Tanzania itatikisika. Sasa mbona hakuna tikisiko lolote?

  ReplyDelete
 10. He is very arrogant, he thinks he is the only one with those qualifications?

  ReplyDelete
  Replies
  1. He's one in a million,kwa achievements zake ktk hii wizara na muda aliokaa,inapita miaka ya mawaziri wote since independence. So Yes!to ur question,his qualifications and his delivery is beyond measure!!!!Only The Lord above can repay for his sweat&commitment for his country after the sacrife of giving up his six figures income he had abroad!!!MHE. MUHONGO!!Keep ur head up!!!wenye uelewa wa nchi inavyoendeshwa wengi wetu tuko nyuma yako tunakuombea!!!mashabiki wa siasa wengi wao ni mangumbaro,wamedandia siasa ukubwani!!!!Kaa ukijua kuwa hata MITUME HAWAKUKUBALIKA KWAO!!!!!MAY GOD BLESS U OUR DEAR BROTHER!!!!!!!

   Delete
 11. This Prof Muhongo is a great guy and was wonderful assert to our country.But Greed people scarified him for their own political benefits. I feel so bad for my country bad people survive and good people have no chance to serve that nation. I wish the greatest to prof Muhongo, but I am glad you're still living, other greatest like Dr. Mgimwa, Sokoine and Nyerere are no longer there, remember that is just a political accident, continue fighting for the poor. God bless you those people will experience their hell while still living in this world.

  ReplyDelete
 12. nadhani muheshimiwa anajisahau kuwa watu hawawezi kuchoka kuzungumza suala la rushwa Tanzania, inatuathiri wote na kujadili escrow ni njia moja ya kutatua tatizo la rushwa, siamini kama ni kupoteza muda, wanaopoteza muda ni hao wahusika ambao hawataki kuachia ngazi wakati vitu viko clear...cheo ni dhamana nadhani tukumbuke hilo, na hongera sana muheshimiwa kwa kuchukua uamuzi sahihi wa kujiuzulu, suala la mijadala ya rushwa litaacha kuzungumziwa iwapo na wengine wote wanaohusika ktk rushwa hii watachukua uamuzi sahihi. Kwa mtazamo wangu bado utaendelea kuwa mbunge na hakuna atakayewadai hela , kujiuzulu ni hatua ya ujarisi na uadilifu, hongera sana mheshimiwa mbunge.

  ReplyDelete
 13. Prof Hongera ! Wewe sio mwana siasa ,Tanzania haiwezi pata viongozi ambao niwachapa kazi na makini kama wewe.Sera zako zina ziba ulaji wa watu.Tumefaidika vipi na Madini si yalikuwepo miaka yote?! Kama sio mikataba feki ya kitoto, tunashindwa na Nchi kama Botswana na Namibia.Binafsi Nakupongeza kwa uamuzi wako, na ninajua Nchi nyingi zinakutambua uwezo wako wa ufanyaji kazi.

  ReplyDelete
 14. This guy is a presidential material.

  ReplyDelete
 15. TWILA KAMBANGWAJanuary 25, 2015

  Jamani mnao sema kwamba ardhi ya tanzania haijatikisika akiachia madaraka inamaana hamuoni? angalieni kule msimbati ambako ndiko chimbuko la hiyo gas ardhi ilivyotikisika na kumung`oka, pumzika kwa amani ndugu muhongo indelea na majukumu mengine achana na wachimba chumvi

  ReplyDelete
 16. I hear you Prof Muhongo! Mimi kama watanzania wengi tu napenda kuwa na watu wenye sifa kama ulivyojieleza kushika dhamana ya juu ya uongozi wakiwa na nia kuu moja tu, ambayo ni kuondoka umaskini kwa watanzania. Ni kweli tunataka wasomi wanaochukia rushwa na ufisadi na ambao wanaweka mbele maslahi ya taifa kuliko maslahi binafsi. Tunataka viongozi wanaoheshimu mawazo ya kila mmoja bila kubagua yanatoka Chana gani, ama kutoka kwa mtu wa ngazi ipi au Hali gani ya kimaisha mradi mawazo yao yanajenga katika kuboresha maisha ya mtazania hasa wa hali ya chini.

  Mimi binafsi ninekuelewa ulivyojieleza na huenda ukiwa kweli hayo unayosema kuwa watu wanakusakama kutoka a na issue zao binafsi ukiwa ni pamoja na wivu na fit a.

  Mimi ni mmoja wa Watu ambao bado sijaelewa kwa nini wewe usuluhishe hizo two parties kama unavyosema kwa nia njema na bila kupata chochote lakini matokeo ya usuluhishi huu usababishe kikundi cha watu wagawiwe mabilioni ya shilingi bure tu, so kwamba ni mokpo au nini, ni bure tu watu wapokee mabilioni ya shilingi, wakati watanzania wanaishi katika umaskini wa Hali ya juu.
  Unasema umeleta maendeleo ya umeme kwa asilimia arobaini na kitu, lakini Mimi najiuliza kama hizo pesa za Escrow zingetumika kuleta maendeleo badala ya kupewa watu wachache mafanikio haya yangekuwa asilimia ngapi zaidi? Umetaja kuwa katika ziara zao vijijini watu hawaulizii Escrow, Bali wanataka maendeleo, ukiwaambia hao wanakikijiji kuwa hizo pesa za escrow zingeweza kuleta maendeleo gani in excess ya hayo waliyonayo, sifikirii kama hao wanakijiji wazazi gums nawe lugha moja.

  Ni kweli inasikitisha kukupokea wewe kama walivyokuwa viongozi wengine waliojiuzulu kisiasa pamoja na utendaji wao uliiotukuka, ni muhimu ili history ikae vema upande wako uwaelezee watanzania kwa nini uliiona ni muhimu kuchukua hiyo role ya usuluhishi iliyosababisha watu kupewa fedha kiholela na kama tunavyosikia pesa nyingine haziko even documented zilikoenda na kuwa zilichukuliwa in cash. Kwa nini pamoja na kupewa muda wote huo TANESCO haikuweza kufikia mwafaka mpaka uamuzi wa mahal ama. Na role yako ilikuwa ni ipi katika kufanya TANESCO ipate haki yake kabla ya uamuzi huo wa mahakama. Kwangu hujawa off the hook yet, bila juju I hayo maswali.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...