Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mawaziri na manaibu waziri aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam jioni hii.Wanne kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue
Moja wa Sura mpya katika baraza jipya la Mawaziri Naibu Waziri wa Elimu Anne Kilanngo Malecela akila kiapo Mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na Freddy Maro
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akizungumza na vyombo vya habari jioni hii wakati akitangaza mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, Ikulu,  Jijini Dar es Salaam leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo ametangaza mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri,ambalo Ameliapisha jioni hii Ikulu,Jijini Dar es Salaam.

Akitangaza uteuzi huo muda mchache kabla ya Mawaziri hao kuapishwa, Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue amesema uteuzi huo unahusu pia kujaza nafasi mbili zilizoachwa wazi na Profesa Anna Tibaijuka Na Profesa Sospeter Muhongo.

Profesa Tibaijuka, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alieachishwa kazi kutokana na kuhusika kwake katika sakata la akaunyti ya Tegeta Escrow.

Kwa upande wa Profesa Muhongo aliachia ngazi mwenyewe mapema leo,  kwa kile alichotaja kuipisha Serikali iendelee kuwatumikia Wananchi badala ya kuendelea na malumbano ya Escrow.

Katika mabadiliko hayo,sura mpya za manaibu mawaziri zimeingia na baadhi ya mawaziri wamehamishwa wizara.

Akitangaza Mabadiliko hayo,Balozi Sefue aliwataja mawaziri hao kama ifuatavyo.

MAWAZIRI
1. Mh. George Simbachawene - Waziri wa Nishati na Madini
2. Mh. Mary Nagu - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mahusiano na Uratibu)
3.Mh. Christopher Chiza - Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji
4. Mh. Harrison Mwakyembe - Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
5.Mh. William Lukuvi - Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
6.Mh. Steven Wasira - Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika
7.Mh. Samwel Sitta -Waziri wa Uchukuzi
8.Mh. Jenista Muhagama - Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge

MANAIBU WAZIRI
1. Stephen Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais - Muungano
2. Mh. Angela Kairuki -  Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
3. Mh. Ummy Mwalimu - Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
4. Mh. Anna Kilango - Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
5 . Mh. Charles Mwijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Jamani kuna watu hapo tuliwazoea, walikua wanaendana na uongozi wao

    ReplyDelete
  2. Prof Muhongo vipi mbona ardhi ya Tanzania bado haijatikisika?

    ReplyDelete
  3. Wasira bado waziri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...