Na Happiness Katabazi (UB)


MAKAMU wa Rais ,Dk.Mohammed Gharib Bilal anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekwaji wa jiwe la Msingi la Chuo Kikuu  Cha Bagamoyo(UB), zitakazofanyika Jumamosi Januari 17 katika Kijiji cha  Kiromo, Bagamoyo Mkoani Pwani.


Akizungumza na waandishi wa Habari  ofisini kwake Mikocheni Dar es Salaam, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia Fedha na Utawala, Dk.Elifuraha Mtalo  alisema  sherehe hizo zitafanyika Katika Kijiji cha Kiromo    na kwamba uwekwaji wa jiwe hilo ni ufunguzi rasmi wa ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo Katika Kijiji hicho ambao unatarajiwa  kuanza Mwaka huu.


Dk.Mtalo   alisema Dk.Bilal  ndiye atakuwa mgeni rasmi pia na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa naye anatarajiwa kuwa miongoni mwa wageni walioalikwa katika sherehe hiyo ya kihistoria katika Wilaya ya Bagamoyo kwasababu Somo la Historia linatufundisha kuwa  mji wa Bagamoyo watumwa walikuwa wakiishi.


"  UB tunaifahamu historia ya Mji wa Bagamoyo ndiyo maana tukaamua kuanzisha Chuo Kikuu ambacho tumekipa jina la University of Bagamoyo.Kupitia   Mji wa Bagamoyo tulikuwa watumwa, hivyo kupitia   UB  ambayo inajenga makazi yake ya kudumu   katika mji huo, binadamu wote watakuwa  huru kwasababu tutapata elimu" alisema Dk.Mtalo.


Alisema UB ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2011 ambayo ina makazi yake yake ya muda ,Mikocheni  B, Dar es Salaam  na kwamba ujenzi wa Makazi ya kudumu ya UB kijijini Kilomo , utasaidia kukuza shughuli za uchumi, wananchi wa eneo hilo kupata huduma ya elimu ya ngazi ya Chuo Kikuu kwa ukaribu na ajira.

Aidha aliwaomba wananchi Wilaya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kujitokeza kwa Wingi Katika sherehe hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...