Pichani juu na chini ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia Baadhi ya wakazi wa mji wa Kizimkazi waliofika katika uwanja wa Kizimkazi Mkunguni,Wilaya ya Kusini Unguja kumsikiliza.Ndugu Kinana ambaye leo anaikamilisha ziara yake ya siku kumi katika kisiwa cha Unguja akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,katika suala zima la kuimarisha uhai wa chama na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
Mkutano wa hadhara ukiendelea katika uwanja wa Kizimkazi mkunguni,Wilaya ya Kusini Unguja mapema leo jioni.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikabidhi majiko ya gesi kwa vikundi vya akina mama wa Makunduchi yaliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Makunduchi,Mh.Samia Suluhu na Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi,Mh Haroun Ali Suleiman.
Ndugu Kinana akishiriki kupandisha mabomba kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa Kibuteni-Makunduchi unaosaidiwa na jumuiya ya Milele Zanzibar Foundation.Pichani shoto ni Afisa Maji Mkoa wa Kusini Unguja,Bwana Hafidhi Hassan  Mwinyi,ambaye alisema kuwa lengo la Mradi huo ni kuhuwisha,kuiimarisha na kuikuza miundombinu ya maji safi na salama ya Makunduchi Kibuteni ili iweze kutoa huduma vizuri na kwa ubora unaohitajika kwa walengwa wake.Mradi huo unakisiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 650 na ushehe.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na wanachama wengine,wakiwaongoza wanachama wapya wapatao 518 kula kiapo mara baada ya kujiunga na chama hicho sambamba na kukabidhiwa kadi za uanachama.
Baadhi ya wakazi wa mji wa Kizimkazi wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa Kizimkazi Mkunguni,Wilaya ya Kusini Unguja kwa minajili ya kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ambaye leo anaikamilisha ziara yake ya siku kumi katika kisiwa cha Unguja akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,katika suala zima la kuimarisha uhai wa chama na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...