Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Dkt. Asha-Rose Migiro akimtunuku shahada ya uzamili ya usimamizi wa miradi mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda katika mahafali ya 27 ya chuo hicho yaliyofanyika mjini DODOMA. Kushoto anayeshuhudia ni Makamu mkuu wa chuo hicho Profesa Tolly Mbwete.

Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda  akitoka kupokea shahada ya uzamili ya usimamizi wa miradi. Akiongea baada ya hapo Mama Pinda ametoa wito kwa kinamama wa Tanzania na Afrika kwa jumla kujiendeleza kielimu ili kukomboa mataifa yako kutoka katika dimbwi la umaskini
 Kikundi cha wake wa viongozi kutoka Dar es salaam kikimpongeza mlezi wao Mama Tunu Pinda kwa kutunukiwa shahada ya  uzamili ya usamamizi miradi ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania katika mahafali ya 27 iliyofanyika Mjini Dodoma. Toka  kushoto ni  Mama Mashiba,  Mama Lukuvi na Mama Malima 
Wanafamilia wakimvisha maua Mama Tunu Pinda. Picha na Chris Mfinanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Well done mama, just in case ufesti ledi unakuja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...