THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Rais amteua George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu mpya wa serikali


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju (pichani) kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.


3 Januari, 2015


Kuna Maoni 5 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Hongera sana,ndugu Massaju.Cheo hiki umekistahili kwelikweli.WEWE NI JEMBE.

 2. Anonymous Anasema:

  Hongera bwana mzee. Kwa sura unaonekana kama mtu serious na kazi yako. Tafadhali simama imara na hudumia nchi yako kwa uaminifu na piga vita ufisadi.

 3. Al Musoma Anasema:

  Mwanasheria mkuu wa serikali mpya
  Mwanasheria mkuu mpya wa serikali

  Mwalimu wangu wa Kiswahili darasa la pili (Mrs Uledi) angalijua tofauti

 4. Anonymous Anasema:

  Hongera sana AG Masaju.Endelea na Falsafa yako ya kuheshimu,kuamini na kuthamini viwango na uwezo wa kitaaluma wa mtu bila kujali umri au ngazi ya afisa husika.falsafa yako hiyo ndiyo iliyokufikisha hapo.

 5. Anonymous Anasema:

  Huu msemo, "WEWE NI JEMBE" maana yake nini. Naomba kuelimishwa.