Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju (pichani) kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.


3 Januari, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hongera sana,ndugu Massaju.Cheo hiki umekistahili kwelikweli.WEWE NI JEMBE.

    ReplyDelete
  2. Hongera bwana mzee. Kwa sura unaonekana kama mtu serious na kazi yako. Tafadhali simama imara na hudumia nchi yako kwa uaminifu na piga vita ufisadi.

    ReplyDelete
  3. Mwanasheria mkuu wa serikali mpya
    Mwanasheria mkuu mpya wa serikali

    Mwalimu wangu wa Kiswahili darasa la pili (Mrs Uledi) angalijua tofauti

    ReplyDelete
  4. Hongera sana AG Masaju.Endelea na Falsafa yako ya kuheshimu,kuamini na kuthamini viwango na uwezo wa kitaaluma wa mtu bila kujali umri au ngazi ya afisa husika.falsafa yako hiyo ndiyo iliyokufikisha hapo.

    ReplyDelete
  5. Huu msemo, "WEWE NI JEMBE" maana yake nini. Naomba kuelimishwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...