Mkutano wa Kumi na Tisa wa Bunge la Kumi ambao ni mahusisi kwa ajili ya Kushughulikia Miswada ya Sheria, unatarajiwa kuanza siku ya Jumanne tarehe 17 Machi 2015 na kumalizika tarehe 1 April 2015 Mjini Dodoma. Shughuli zitakazokuwepo katika Mkutano huo ni kama ifuatavyo:

1.0        MISWADA YA SHERIA:
1.1        MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI:
a)   Kusomwa kwa mara ya Kwanza na hatua zake zote:
Katika Mkutano huo, Kwa mujibu wa Kanuni ya 93(3) ya Kanuni za Bunge Toleo la Aprili 2013  Jumla ya Miswada Sita (6) itawasilishwa Bungeni kwa Hati ya Dharura na inakusudiwa kupitishwa na Bunge katika hatua zake zote. Miswada hiyo ni:
(i)       Muswada wa Sheria ya kupata habari wa Mwaka 2015(The Access to Information Bill, 2015),
(ii)      Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari wa   Mwaka 2015 (The Media Services  Bill, 2015),
(iii)     Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa Mwaka 2015 [The Fair Competitio (Amendment) Bill, 2015],
(iv)     Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao wa Mwaka, 2015(The Computer and Cyber Crimes Bill, 2015),
(v)      Muswada wa Sheria ya Miamala ya Kiektoniki wa Mwaka 2014 (The Electronic Transaction Bill, 2015),
(vi)     Muswada wa Sheria ya Gesi Asilia wa Mwaka 2015 (The Natural Gas Bill, 2015).
b)   Kusomwa kwa mara ya Pili na hatua zake zote:
Aidha, Jumla ya Miswada 15 itasomwa kwa mara ya Pili Bungeni na kupitishwa na Bunge katika hatua zake zote kwa mujibu wa Kanuni ya 86(1) ya Kanuni za Bunge. Miswada hiyo ni:
(i)       Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Ajira za Wageni wa Mwaka 2014 [The Non- Citizens Employment Regulation Bill, 2014];
(ii)      Muswada wa Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa  wa Mwaka 2015 [The National Payment Systems Bill, 2015],
(iii)     Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa Mwaka 2014 (The Tax Administration Bill, 2014.
(iv)     Muswada wa Sheria ya Takwimu wa Mwaka 2014 (The Statistics Bill, 2014),
(v)      Muswada wa Sheria ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI wa Mwaka 2014 [The Tanzania Commision for AIDS (Amendment) Bill, 2014],
(vi)     Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa wa   Mwaka 2014 [The Disaster Management Bill, 2014],
(vii)    Muswada wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Dawa za Kulevya wa Mwaka 2014 [The Drug Control and Enforcement Bill, 2014],
(viii)   Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Stakabadhi Ghalani wa Mwaka 2014 [The Wharehouse Receipts (Amendment) Bill, 2014],
(ix)   Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji wa     Mwaka 2014 [The Immigration (Amendment) Bill, 2014],
(x)       Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Silaha wa Mwaka  2014 [The Firearms and Ammunition Control Bill, 2014],
(xi)    Muswada wa Sheria ya Wataalam wa Kemia wa    Mwaka 2014 [The Chemist Professionals Bill, 2014],
(xii)    Muswada wa Sheria ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka 2014 [The Government Chemistry Laboratory Bill, 2014],
(xiii)   Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2014 [The Written Laws (Miscellaneous Amendements) (No. 2) Bill, 2014] ,
(xiv)  Muswada wa Sheria ya Bajeti wa Mwaka 2014 [The Budget Bill, 2014], na
(xv)   Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania wa Mwaka 2015 [The Youth Council of Tanzania Bill, 2015],

1.2        MUSWADA BINAFSI WA MBUNGE:
kwa Mujibu wa kanuni ya 81 (1) ya Kanuni za Bunge, katika Mkutano ujao wa 19 kunatarajiwa kuwasilishwa Muswada Mmoja wa Mbunge Binafisi ambao ni Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana la Taifa wa Mwaka 2013 (The Nationa Youth Council Bill, 2013) wa Mheshimiwa John John Mnyika. Muswada huu utasomwa kwa mara pili na hatua zake zote.

2.0        MAAZIMIO NA ITIFAKI MBALIMBALI
Pamoja na Miswada hiyo, katika Mkutano wa 19, Bunge linatarajia pia kuazimia Maazimio Mawili kama ifuatavyo:
1.        Azimio la kuridhia Mkataba wa Msingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala Barani Afrika.
2.        Azimio la kuridhia Makubaliano ya Msingi ya Ushirikiano katika Bonde la mto Nile (Agreement on the Nile river basin Co-operative Framework- CFA).

3.0       MASWALI:
Aidha, katika Mkutano huu  wa 19 wa Bunge, Jumla ya Maswali ya kawaida 170 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa ambapo ni wastani wa Maswali 15 kwa siku na maswali 10 kwa siku za Alhamisi.
Aidha kutakuwa na kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu kwa Mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ambapo jumla ya  Maswali 18 ya msingi yataulizwa na kujibiwa na Mhe. Waziri Mkuu. 
Ratiba Kamaili ya Mkutano wa Kumi na Tisa (19) na jinsi shughuli zitakavyowasilishwa itatolewa baada ya Kamati ya Uongozi kukutana Jumatatu tarehe 16 Machi, 2015 ambapo itatolewa na kuwekwa katika Tovuti ya Bunge ambayo ni  www.parliament.go.tz

Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi Ndogo za Bunge
DAR ES SALAAM

13 Machi,  2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...