IMG_8515
UMOJA wa Vyama vya wanafunzi Elimu ya juu kutoka vyuo mbalimbali kanda ya kaskazini Kilimanjarona ,Arusha ,wajitokeza kumshawishi Prof. Sos peter Muhongo Kugombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania  Mwaka 2015.(Picha na Jamiiblog).
IMG_8521Akizungumza kwa niaba ya vijana wenzake Mwenyekiti wa vijana hao Charles Ngereza kutoka chuo cha uhasibu Arusha amesema kuwa kinachowafanya kumshawishi prof Sos peter kugombea urais ni kutokana na kuwa kiongozi bora kwa wananchi na mtu anayejali matatizo ya wananchikatika kuwapatia huduma
IMG_8509
Pia wanasema kuwa amekuwa akiwezesha  uchumi kujitegemea na kupinga ulanguzi katika sekta ya uwekezaji pamoja na kutetea vijana katika uwekezaji na kupata ajira.
IMG_8515
Vijana hao ambao ni umoja wa vyama vya wanafunzi wa elimu ya juu katika picha kutoka kushoto ni NELSON WILSON MACHUMU ,TUMAIN UNIVARSITY. 2 DAUD HIPOLITY SHAYO CHUO CHA UHASIBU (IAA)3 SARAH AMINIRABI MUSHI ARUSHA UNIVARSITY 4CHARLES NGEREZA CHUO CHA UHASIBU  ARUSHA.5HOBESHIJUVENARY MAKUMIRA UNIVARSITY PAMOJA NA RAHMA YUSUPH SENGEZA CHUOCHA JOMO KENYATA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hakuna rangi hatutaona mwaka huu.Hata rangi za rainbow zinasingiziwa.

    ReplyDelete
  2. Mwandishi ungeandika umoja wa vyama vya wanafunzi wa elimu ya juu kutoka mkoa wa Arusha sio kanda ya kaskazini kwa vile sijaona muwakilishi kutoka chuo cha elimu ya juu chochote kilichopo mkoa wa Kilimanjaro. Itawezekanaje viongozi wa vyama hivyo wa kanda watoke mkoa wa Arusha tu wakati Moshi kuna vyuo kama Chuo kikuu cha ushirika, Chuo kikuu kishiriki cha kumbukumbu ya Stefano Moshi na chuo kikuu kishiriki Mwenge? Hao wamekurupuka?

    ReplyDelete
  3. Bila shaka kwa mantiki ya uhuru wa kutoa maoni..............NATUMIA FURSA YA JUKWAA HILI KUUNGA MKONO HOJA HII ya Prof. kujitosa kwenye ulingo wa kinyang'anyiro cha 2015.

    ReplyDelete
  4. UNIVARSITY UNIVARSITY UNIVARSITY ndo nini ?

    ReplyDelete
  5. Hawa nao sijui wametumwa na nani? Huu ni mwaka wa viroja vitupu

    ReplyDelete
  6. Hahaha ndio wasomi wetu hawa, kazi ipo haswa na bado mnalalamika kwanini tunawaajili wakenya na waganda na kuwasahau nyinyi. Noana wanyarwanda nao wameanza kuja vizuri sana.

    Hongereni wasomi wetu.

    ReplyDelete
  7. Hao wanasoma UNIVERSITY au UNIVARSITY???? Ama kweli kama ni hivyo wana haki ya kumuomba professor wao bwana Muongo. Na huyo wa Kenyatta univ. anamwakilisha nani? Watanzania nao kwa kujaribu mambo? Lakini ndiyo mambo ya uhuru wa kusema, ningewashauri wawe clear kwenye hilo walifanyalo waweke objectives zao chini. ANGALAU WAMEJARIBU KUONYESHA NYUSO ZAO.

    ReplyDelete
  8. KWA KILA ANAEPATA WADHIFA,AKAIBA,KESHO ANAGEUKA KUWA HERO. ONLY IN TANZANIA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...