Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Balozi Liberata Rutageruka Mulamula (kulia) kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 

Kwa sasa Balozi Mulamula ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico.


Rais Kikwete pia amemteua Balozi Hassan Simba Yahya (chini) kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  


Kwa sasa Balozi Yahya ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizarani hapo.



Uteuzi huu umeanza tarehe 2 Mei, 2015


Imetolewa na;
Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.
4 Mei, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2015

    Hongera Balozi na Yayha kwa uteuzi huu.

    ReplyDelete
  2. Hongereni sana Mama Mulamula na Bwana Yahaya kwa uteuzi huu!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2015

    kiukweli mna bahati marekani kuwa na balozi kama huyo anayejitkeza hata kwenye mikusanyiko ya watanzania...ila wenzenu huku Canada kikwete anakosea mabalozi tokakamtoa khalage kumekuwa kimya ila nasikia kuna balozi mwingine kaja wenda akawa mzuri.ni shidaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...