Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF) limeendelea na zoezi la upimaji afya kwa wananchi, Zoezi hili lililoanzia mkoani Tanga limeendelea kwenye manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Zoezi lililofanyika kwa siku tatu mfululizo limekuwa la mafanikio kwa kuweza kuwafikia watu zaidi ya 900 .
Huduma zilizo kuwa zikitolewa kwenye zoezi ni pamoja na:
Upimaji wa Shinikizo la damu
Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari
Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa uzito)
Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na Matatizo 
Ushauri nasaha  na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI)
Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji wa Afya.
Uchangiaji wa damu kwa Hiari.

Huduma  zote hizi zitatolewa na NSSF, BURE.
NSSF inaendelea kuwasii na kuwahimiza wakazi wa Manispaa ya Moshi kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI Scheme. NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji wadogo, Wavuvi,  Ushirika wa Bodaboda , Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.
Jiunge na NSSF HIARI Scheme ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS,  pamoja na Mafao bora mengineyo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji NSSF Bw. Crescentius Magori akipima sukari wakati wa zoezi la upima Afya katika Viwanja vya Memorial, Manispaa ya Moshi.
Wakazi wa manispaa ya Moshi wakipima VVU kwa Hiari Kwenye zoezi la Upimaji Afya linaloendeshwa na NSSF.
Daktari Aisha wa NSSF akimpima shinikizo la damu mkazi wa manispaa ya Moshi kwenye zoezi la upimaji Afya bure kwa wakazi wa manispaa ya Moshi.
Dkt. Zakia kutoka NSSF akimpima mkazi wa manispaa ya Moshi Shinikizo la Damu wakati wa zoezi la upimaji Afya bure lililoandaliwa na NSSF.
Wakazi wa Manispaa ya Moshi wakiwa wamejitokeza kwa wingi ili wapime Afya zao na kujua hali zao za Lishe kwenye zoezi lililoandaliwa na NSSF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...