Kufuatia mgogoro  wa kisiasa, jaribio la kumtoa madarakani Raisi wa Jamhuri ya Burundi, Pierre Nkurunziza na maelfu ya wananchi wa nchi hiyo kukimbilia nchi jirani za Tanzania na Rwanda. Hali ya kambi zinazopokea wakimbizi zinaonekana kuelemewa na kupelekea kuhatarisha hali za wakimbizi hao.

Kutokana na hali hiyo, Bunge la Afrika ya Mashariki kupitia kamati yake ya Masuala ya Jumuiya na Usuluhishi wa Migogoro imeteua wajumbe watakaokwenda kutembelea kambi hizi zilizopo Kigoma-Tanzania na Mashariki mwa nchi ya Rwanda kwa madhumuni yafuatayo;

1.     Kujiridhisha na hali ya mazingira ya kambi hizo na kuangalia mipango kutatua mgogoro huo.
2.     Kuangalia na kutimiza jukumu la Bunge la Afrika Mashariki kupata suluhisho la kudumu la mgogoro ulioko sasa nchini Burundi.
3.     Kuwatemebelea na kuwafariji wananchi wote wa Burundi walioko kwenye kambi hizo.

Wajumbe wa kamati teule wamegawanyika katika makundi mawili, wajumbe watakaokwenda Kigoma-Tanzania wataongozwa na Mhe. Abdullah Mwinyi ambae ni menyekiti wa kamati hiyo na wajumbe watakaokwenda Mashariki mwa Rwanda wataongozwa na Mhe. Abubakar Zein.

Imetolewa na;
Mhe. Abdullah Mwinyi
(Mwenyekiti wa Kamati ya masuala ya Jumuia na Usuluhishi wa Migogoro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...