PROGRAMU
mpya za utamaduni na ubunifu zinatoa fursa kubwa ya uanzishaji wa
shughuli za kitamaduni zenye kuimarisha sekta ya ubunifu wenye mwelekeo
kiuchumi.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania,Bw. Johnny Flentoe akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa program mpya ya CKU.
Kwa
mujibu wa balozi wa Denmark nchini Tanzania,Bw. Johnny Flentoe, amesema kwamba
Tanzania inautajiri mkubwa wa kiutamaduni ambao unaweza kutumiwa kuchangia pato
la taifa GDP.
“Bado tasnia ya sanaa
na ubunifu ambayo ingeliweza kuchangia katika uchumi na kuwapatia kazi vijana
haijatumika ipasavyo. Kutokana na hilo kipaumbele cha programu hii mpya ni
kuwezesha vijana kutumia sanaa na ubunifu kukuza ajira,” anasema balozi Johnny
Flentoe.
Mshairi Jasper Sabuni akifanya kazi ya 'spoken words' wakati wa uzinduzi wa program mpya ya CKU.
Juni 5, 2015, Ubalozi wa
Denmark ukishirikiana na Kituo cha Utamaduni na Maendeleo cha Denmark (CKU) umezindua
program mpya ya utamaduni na maendeleo Tanzania ( Tanzania Culture and
Development Programme ).
Programu hiyo imelenga
kutengeneza fursa za kiuchumi kupitia jukwaa la sanaa na ubunifu ambapo
watanzania watajipambanua kupitia kushiriki shughuli mbalimbali za kitamaduni
na kujipatia kipato.
Baadhi ya wadau waliofika kwenye uzinduzi wa program mpya ya CKU Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja
CKU
inatekeleza program hiyo kupitia kwa washirika wake likwemo Tamasha la
Kimataifa la Filamu (Zanzibar International Film Festival (ZIFF), kupitia mradi wao
wa Village Panorama ambao unalenga kuonyesha filamu za kuelimisha maeneo ya vijijini
huko Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...