WAZIRI wa zamani wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo, ametangaza nia rasmi ya kuwaomba Wana CCM kumteua kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba, huku akisema ni yeye pekee mwenye uwezo wa kuikwamua nchi katika hali mbaya ya umasikini na ukosefu wa wataalamu, hali inayoifanya nchi ishindwe kupiga hatua.

Pamoja na mambo mengine, Muhongo alitumia muda mwingi kutoa takwimu hali ya umasikini na utajiri kwa wananchi wa Tanzania, bila kusahau baadhi ya nchi ambazo zimeweza kupiga hatua kubwa kwa kujikita kwenye kuzalisha wataalamu na watafiti, akiwamo yeye, ambaye si tu ni Profesa, bali pia amebobea kwenye nishati kwa miaka mingi.

Akizungumza kwa kujiamini mbele ya wanachama wa CCM na Watanzania katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria, Musoma Mjini, Profesa Muhongo alisema kwamba anayo tiba ya umasikini wa Watanzania kwa kuhakikisha kwamba anatumia utaalamu wake kwa kusimamia mambo ya gesi, mafuta, umeme, bila kusahau elimu kwa ajili ya kuwakwamua wananchi wake.

“Nchi ina upungufu mkubwa wa takwimu hali inayowafanya viongozi washindwe kujua namna gani wanaweza kuondoa umasikini na kero zinazowakumba wananchi wake, hivyo hata wale wanaosema wanataka uongozi, hawajui wangapi wenye uhitaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2015

    kweli wewe umesema ukweli utawatolewa watanzania umasikini kama ulivyowaondolea umasikini watu wa kijijini kwako. Tutakuchaguwa tu bwana prof.nyinyi ndiyo wasomi munaotuendeshea nchi vizuri.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 02, 2015

    Nauhakika hapa Raisi tumeshampata. Kura yangu inasuburi tarehe tu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 03, 2015

    Hacheni ndoto za mchana hapo juu, Urais sio kuwa balozi wa nyumba 10! Tanzania inahitaji Rais atakae leta maendelel kwa Taifa na kulinda maslahi na Resoirces za Taifa la Tanzania.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 03, 2015

    Kwa kipindi hiki,nchi yetu inamhitaji sana huyu Mhe. na tuachane na siasa. Tukiweka Team ya Muhongo,Nchemba tutakuwa tuko serious. Ila kawaida yetu kufanya ushabiki halafu tunajuta

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 03, 2015

    Huyu si ndo yule anayesema wazawa hatuna uwezo wa kushuriki kwenye uzalishaji? Yaani kumiliki viwanda? Sasa umasikini atautoaje? Maana tunachohitaji sio kuondoa umasikini, tunachohitaji ni utajiri! Na huwezi kuupata utajiri kwa kutumikishwa tu kwenye makampuni ya wageni! Tayari hapa ashakosa kura yangu!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 03, 2015

    Hili ni jembe, kazi za takwimu sio blah blahhhh, maendeleo 0 kila siku. Tumuingize ikulu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...