Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
JAMII imetakiwa kutambua mahitaji ya watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea  katika kubaini  changamoto zao katika maisha wanayoishi na kuweza kuguswa kutoa msaada.
Hayo ameyasema leo Mhasibu Mwandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Idara za Serikali na Mabalozi,Wema Mbaga wakati akitoa msaada wa kituo Khilati Kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam,amesema kuwa wanatambua umhimu wa kutoa msaada kwa makundi maalumu wakiwemo watoto wanaolelewa katika vituo.
Amesema kuwa watoto wanachangamoto nyingi katika ukuaji wao ikichangiwa na kuondokewa na wazazi wao hivyo wanahitaji faraja kutoka kwa jamii katika kuweza kufikia ndoto zao.
Wema amesema watu wengine wanawajibu kuwakumbuka watoto katika katika kipindi hiki cha kuelekea Siku Kuu ya Idd El-Fitri kuwaza kupata mahitaji yao.
Vitu walivyotoa ni Magodoro ,Daftari,Kalamu ,vyenye thamani y ash.milioni 1.5 ambapo ni sehemu ya mchango wao.
Mkurugenzi wa Kituo hicho ,Khadija Hussein  amesema kutuo kinachangamoto ya eneo kwani eneo waliopo watoto wanalipia kodi pamoja na matatizo ya chakula.
Amesema watu wenye uwezo watembelee kituo hicho na kuona mahitaji yao ili waweze kusaidia katika kulea watoto hao ambao wako 65.
Mhasibu Mwandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Idara za Serikali na Mabalozi,Wema Mmbaga akitoa akikabidhi msaada kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto Yatima cha  Khayrat  Kilichopo ,Kigogo,Khadija Hussein katika hafla iliyofanyika kituo hicho ,jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto Yatima cha  Khayrat,Khadija Hussein akizungumza na waandishi wa habari juu ya msaada walioupata katika hafla iliyofanyika kituo hicho ,jijini Dar es Salaam.
 Mhasibu Mwandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Idara za Serikali na Mabalozi,Wema Mmbaga akizungumza na waandishi wa habari juu ya msaada walioutoa katika kituo cha kulele watoto yatima cha Khayrat, katika hafla iliyofanyika kituo hicho ,jijini Dar es Salaam.  
Sehemu ya watoto katika kituo cha Khayrat wakiwa na daftari zilizotolewa na NSSF Mkoa wa Idara za Serikali na Mabalozi katika hafla iliyofanyika kituo hicho ,jijini Dar es Salaam. 
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...