Mkuu wa Biashara za Kibenki, Rahim Kanjii akipeana mkono na Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Chamanzi, Ancent Shayo  mara baada ya kutoa msaada wa meza 25 na  viti 25.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
 BENKI ya NIC imetoa msaada wa madawati 25 katika shule ya msingi Chamanzi yenye thamani ya Sh.Milioni tatu kutokana na shule hiyo kukabiliwa na changamoto ya madawati.

Akizungumza baada ya kukabidhi  madawati  hayo, Mkuu wa Biashara za Kibenki,Rahim Kanjii amesema kuwa shule hiyo waliona ina umhimu wa kusaidiwa sehemu ya madawati katika kupunguza idadi ya wanafunzi wanaokaa chini ardhi wakiwa darasani.

Amesema shule hiyo inatakiwa kusaidiwa kwa kila hali kwani watoto wanaoandaliwa kuwa taifa la kesho hivyo wanatakiwa kuandaliwa mazingira bora ya kupata elimu.

Kanji amesema kuwa ameguswa sana na benki itaendelea kadri ya uwezo wake kusaidia shule katika kuweza kuondokana na chagamoto ya madawati  katika kujenga mazingira bora ya kusomea watoto kwani wanaandaliwa kuja kuwa wanataaluma mbalimbali.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Ancent Shayo amesema kuwa shule ina wanafunzi 3200 lakini vyumba vya madarasa 11 na kufanya kila darasa kukaa wanafunzi 150.

Amesema madawati hayo ni kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nne kutokana na kupungukiwa madwati 175 ambapo NIC imepunguza imetoa madawati 25 hivyo kwa darasa hilo linahitaji madawati 150 ili waweze kukaa katika siku ya mtihani wa taifa.

Shayo amesesema hitaji katika shule licha ya madawati wanaupungufu wa vyumba vya madarasa  kutokana na idadi ya wanafunzi hao.

 Wanafunzai wa shule ya msingi Chamanzi wakiwa darasani wakiwa wamekaa chini kwa kutokuwa na madawati ya kutosha katika chumba cha darasa la tatu walipotembelewa na wafanyakazi wa Benki ya NIC leo jijini.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Chamanzi, Ancent Shayo akizwa na wafanyakazi wa Benki ya NIC walipowatembelea wanafunzi wa Shule ya Msingi Chamanzi jijini Dar es Salaam walipotembelea chumba cha darasa la kwanza katika shule hiyo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...