Wananchi wanaotembelea maonesho ya Kilimo na mifugo Nananane Njiro jijini Arusha wakiwa kwenye banda la Chuo cha Ufundi Arusha kupata maelezo ya namna kinavyotimiza wajibu wake kuelimisha vijana katika taaluma ya ufundi nchini.
Wanafunzi na wananchi wakipata maelezo kutoka kwa Mkufunzi wa Mitambo,Frank Moshi kwenye banda la Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)juu ya matumizi ya nishati ya Nguvu jua.
ATC pia hutoa mafunzo ya kuongeza thamani madini  hapa nchini badala ya kusafirishwa yakiwa ghafi kwa kuchakata katika mwonekano unaongeza thamani na kuongeza ajira kwa vijana.
Mkufunzi wa Maabara Lemael Anael wa  ATC akimpa maelezo mmoja wa wananchi waliofika kujifunza,Chuo hicho hutoa mafunzo kwa walimu wa maabara katika Shule za Sekondari nchini katika masomo ya Fizikia,Kemia na Bailojia. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...