Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM. Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM.

 MCHUANO wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajia kufanyika Oktoba 25, 2015 unaendelea maeneo mbalimbali ya nchini, huku vyama anuai vilivyofanikiwa kuingia katika ushindani huo wa kisiasa vikinadi ilani na sera zao kwa Watanzania ili kuwashawishi wachaguliwe.

 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mara ya kwanza kimemsimamisha mwanamke katika ngazi ya juu ya uongozi. Kimemteuwa mwanamama, Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza wa mgombea wa nafasi ya urais kupitia chama hicho, John Pombe Magufuli. 

Kwa mantiki hiyo endapo kitafanikiwa kushinda urais Tanzania kwa mara ya kwanza mwanamke atashika nafasi ya juu ya madaraka ndani ya Serikali. Bi. Suluhu ambaye amewahi kufanya kazi kama kiongozi katika Serikali zote mbili yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar (Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar-SMZ) anauzoevu wa kutosha na elimu nzuri inayomuongeze sifa ya kuimudu nafasi aliyopewa kwa sasa.

 Ki historia, Bi. Suluhu alizaliwa Januari 27, mwaka 1960 nchini na kupata elimu yake ya msingi na sekondari Zanzibar, kabla ya kuendelea na elimu ya juu kwa kozi mbalimbali katika vyuo vikuu vya Mzumbe nchini Tanzania, Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza kwa ushirikiano na Chuo Kikuu Huri cha Tanzania (OUT). [caption id="attachment_62370" align="aligncenter" width="741"]Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (kulia) akimjulia hali mmoja wa akinamama katika moja ya wodi za wazazi nchini. Kiongozi huyo anaahidi endapo atashinda uchaguzi kupitia chama chake ataziangalia zaidi huduma za afya ya uzazi ili kuboresha zaidi. Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (kulia) akimjulia hali mmoja wa akinamama katika moja ya wodi za wazazi nchini. Kiongozi huyo anaahidi endapo atashinda uchaguzi kupitia chama chake ataziangalia zaidi huduma za afya ya uzazi ili kuboresha zaidi.

 Mwanamama huyu pia amefanikiwa kuchukua kozi ndogo ndogo anuai katika vyuo vya ndani na nje ya Tanzania, vikiwemo vya; 'Institute of Management for Leaders, Hyderabad, India', Zanzibar Institute of Financial Administration, ZIFA, pamoja na National Institute of Public Administration, Lahore Pakistan. Mgombea huyo mwanamama amekuwa waziri na mbunge kwa zaidi ya miaka mitano mfululizo na pia kufanikiwa kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, nafasi ambazo kwa kiasi kikubwa zinamuongezea sifa ya kuweza kuimudu nafasi aliyopewa kwa sasa anasema hii ni nafasi pekee kwa akinamama wote bila kujali itikadi zao kumuunga mkono ili aweze kushinda na kuweka historia nchini ya mwanamke kushika nafasi ya juu kuliko zote nchini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hizi kampeni za kupita mahospitalini si zilishakatazwa na NEC?.au zilikatazwa kwa lowassa na UKAWA tu?eti ankali wewe unasemaje hii hali?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...