Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliyehamishwa kutoka Tanga Mhe. Magalula Said Magalula (katikati) akisalimiana na watumishi wa ofisi yake mpya waliokusanyika kumpokea rasmi nje ya jengo la ofisi hiyo jana tarehe 22 Septemba 2015.

Mkuu Mpya wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Magalula Said Magalula kulia na Katibu Tawala Mkoa huo Ndugu Smythies Pangisa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliyemaliza muda wake Eng. Stella Manyanya ambaye yupo kwenye harakati za kugombea Ubunge Jimbo la Nyasa wakisaini nyaraka za makabidhiano ya ofisi mapema tarehe 22 Septemba 2015.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa wa pili kulia kwa niaba ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya akimkabidhi rasmi nyaraka za makabidhiano ya ofisi Mkuu mpya wa Mkoa huo aliyehamishwa kutoka Tanga Mhe. Magalula Said Magalula kulia jana tarehe 22 Septemba 2015. Wanaoshuhudia kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha na Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Erasmus Rugarabamu.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Magalula Said Magalula akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi yake mpya kufuatia uhamisho wa hivi karibuni kutoka Mkoa wa Tanga. Katika salamu zake alishukuru kwa mapokezi mazuri na kuomba ushirikiano kwa viongozi na watumishi katika kutimiza majukumu ya msingi ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa wa Rukwa. Aliwataka viongozi pamoja na watumishi kutambua majukumu yao ya msingi ambayo ni kutoa huduma bora kwa wananchi, alisisitiza pia juu kilimo bora chenye tija kwa kuwapa wananchi huduma stahiki. Kutokana na kuwepo kwa tishio la Mvua juu wa wastani (Elnino) Mkuu huyo wa Mkoa amewaagiza viongozi wa halmashauri kuwapa wananchi wao tahadhari na kuhakikisha wanaoishi katika mazingira hatarishi wanaondoka na wengine kuboresha nyumba zao.
 Sehemu ya wakuu wa idara walioshiriki kikao hicho cha makabidhiano.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Ndugu Benson Kilangi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Ndugu Hamid Njovu wakishuhudia makabidhiano hayo.

(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...