THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

VYAMA VYA SIASA VIACHE KUINGILIA MASUALA YA TUME

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu,Damian Lubuva akizungumza na makundi maalum  (hawapo pichani)jinsi watashiriki upigaji wa kura Oktoba 25  iliyofanyika Ukumbi wa New Afrika Hoteli jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama Shirikisho la Watu  wenye Ulemavu Mkoa wa Pwani Adam Shaban akizungumza juu jinsi ushiriki katika upigaji kura Oktoba 25 katika mkutanao uliotishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Slaam.
Sehemu ya washiriki wa makundi maalum katika mkutano wa NEC  juu ya ushiriki wa watu wenye ulemavu katika upigaji kura  oktoba 25  uliofanyika leo Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema vyama vya siasa vitangaze sera zao kwa wananchi na sio kuingilia masuala ya utawala wa tume hiyo.

Hayo ameyasema leo,Mwenyekiti wa tume hiyo,Jaji Mstaafu,Damian Lubuva wakati alipokutana na makundi maalum jinsi watavyoshiriki uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,amesema tume inafanya kazi kwa mujibu wa sheria hivyo vyama vya siasa viachie  tume ifanya kazi yake.

Lubuva amesema kuwa vyama vimekuwa vikishughulika na watu hivyo tume itavichukulia hatua za kisheria kutokana  na kukiuka  kwa maadili ya uchaguzi.

Amesema mabadiliko ya uteuzi baadhi ya watendaji NEC ni suala kawaida kutokana watu kujaza nafasi zilizoachwa wazi.
Lubuva amesema Tume haiko tayari kuingiliwa katika masuala yao ya kiutawala kutokana na kile kinachofanyika kiko katika sheria.

Amesema matokeo yatatolewa katika kila vituo na kwa mwaka watatumia siku tatu katika uchaguzi kwa matokeo yote.
Lubuva amesema wakati uchaguzi visionekane vikundi vyovyote katika eneo la kituo cha kupigia kura vikisubiri matokeo.


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Shukrani Michuzi na Timu yako kwa kuielimisha jamii