Mgombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa Tiketi ya CCM Jimbo la Mahonda ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika foleni ya kusubiri kupiga kura kwenye Kituo chake kiliopo Skuli ya sekondari ya Kitope.
 Balozi Seif akipiga kura ya Kumchagua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Bunge ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Kituo chake hapo Skuli ya Sekondari ya Kitope
 Karani wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar akimuweka alama Balozi Seif kuashiria kwamba ameshakamilisha zoezi la Kupiga kura ya kumchagua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Mbunge, Mwakilishi na Diwani
Balozi Seif akizungumza na vyombo vya Habari mara tuu bada ya kumaliza kutumia haki yake ya kupiga kura hapo Skuli ya Sekondari ya Kitope ambapo ndio kwenye kituo chake cha uchaguzi. Picha na OMPR,  ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwa kweli hali inatia moyo mpaka sasa hivi, kwani amani, utulivu na usalama ndio shikilio letu mpaka sasa hivi, naamini mamia ya watu ndani na nje ya nchi na dunia nzima, macho na masikio yao vyote vimeelekea nchini Tanzania kutaka kuona na kusikia ni ipi au nini itakuwa khatma ya uchaguzi huu mkuu, kwani kwa uzoefu wa takriban chaguzi nyingi barani afrika zimekuwa na khitilafu za hapa na pale zinazohusisha suala zima la uvurugaji wa amani na utulivu, chonde chonde watanzania hilo kwetu lisiwepo na Mwenyeez Mungu atulinde na kutusaidia juu ya hilo na kutulindia amani, utulivu na usalama wa nchi yetu na raia wake na kuwa mfano wa pekee na kuigwa ndani na nje ya nchi, kwa bara zima la afrika na dunia kwa jumla. MUNGU IBARIKI AFRIKA NA WATU WAKE NA AMANI ILIYOPO - AMEN.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...