Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (pichani) amewataka wananchi wote wenye haki ya kupiga kura kuhakikisha wanaheshimu maagizo ya Tume ya Uchaguzi ya kuwataka waondoke katika vituo vya kupigia kura mara baada ya kumaliza zoezi la upigaji kura.

Rais Kikwete Amesema kuwa wenye jukumu la kukaa kituoni ni Mawakala wa wagombea na sio wapiga kura wote kama inavyodaiwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa.
Rais Kikwete ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati wa kilele cha Mwenge wa Uhuru kilchoenda sanjari na kumbukumbu ya miaka 16 ya kifo cha Baba wa Tiafa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
“Mlinzi wa uhakika wa kura ni wakala kwani ndiye anayekuwepo wakati wote katika chumba cha kupigia na kuhesabia kura…ni jambo la kushangaza kuona baadhi ya viongozi wa vyama  vya siasa wakiwahamasisha wafuasi wako kubaki vituo mita 100…wanalinda nini? wakati kuna Mawakala ndani” alihoji Rais Kikwete.
Amesema kuwa  ikiwa wapiga kura wengi watabaki vituoni kwa madai ya kulinda kura upo uwezekano mkubwa wa kutokea fujo ambazo zitasababisha baadhi ya watu kuogopa kupiga kura na hivyo kukosa haki yao ya msingi ya kuwachagua viongozi wanaowataka.
Rais Kikwete amesema kuwa ni vema wananchi wenye sifa za kupiga kura kuondoka kwenye  vituo mara baada ya  zoezi hilo , vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yoyote atakaye kaidi agizo la Tume ya Tiafa ya Uchaguzi.
Amesema kuwa watu wenye nia ya kufanya hivyo wasiilazimishe Serikali ifikie uamuzi wa kuchukua hatua kwa kuwa wanaofanya hiyo wana nia  ovu na nchi hii.
Amesesisitiza kuwa nia yao ovu haitafanikiwa kwani Serikali imejipanga vizuri ili kuhakikisha kila mwananchi wenye sifa ya kupiga kura anafanya hivyo bila bughuza yoyote.
Aidha , Rais Kikwete amewaonya wananchi wote wanaonunua na kuuza vitambulisho vya kupigia kura kuacha tabia hiyo la sivyo dhidi yao zitachukuliwa.
Amesema kuwa ni vema kila mwananch akatunza vizuri kitambulisho chake ili siku ya kupiga kura aende katika kituo cha kupigia kura ili kutekeza haki yake ya kidemokrasia.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Ndugu Juma Khatib Chum akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mwenge wa uhuru wakati  wa sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge zilizofanyika katika Uwanja wa Michezi wa Jamhuri mjini Dodoma leo

Mwenge wa Uhuru unaratarajiwa kuzinduliwa mwakani mkoani Morogoro na kilele chake kitakuwa mkoani Simiyu.

Wakati huo huo....

Katika Kilele cha mbio za mwenge wa uhuru , kumbukumbu ya Baba wa Taifa , Mwalimu JULIUS Nyerere na wiki ya vijana Kitaifa, Rais  Jakaya Mrisho Kikwete katika hotuba yake amezungumzia idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura.
Kwa uhakika amesema kuwa idadi ya wapiga kura ni 22,751, 292 kwa upande wa Bara na 503,193 wa Zanzibar.  Hii ndiyo idadi kamili ambayo imo kwenye hotuba ya Mheshimiwa Rais na hii ndiyo idadi kamili kama ilivyotolewa na Tume ya Uchaguzi Tanzania.

Asanteni
 Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Dodoma

13 Oct, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...