TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa (Pichani)anatumia majina matatu kama ifuatavyo: Kassim Majaliwa Majaliwa au Kassim M. Majaliwa.

Tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo, kumekuwa na uchanganyaji wa majina yake na hii ni kwa sababu tangu akiwa chuoni na jeshini, alikuwa akitanguliza kutaja ubini (jina la ukoo) na ndiyo maana ikawa inasomeka Majaliwa Kassim Majaliwa.

Endapo jina hilo litaanza kuandikwa na ubini, litapaswa kutenganishwa na koma kama ifuatavyo: Majaliwa, Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliteuliwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli Novemba 19, 2015 na kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku hiyo hiyo. Aliapishwa Novemba 20, 2015 kwenye Ikulu ndogo ya Chamwino, Dodoma.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATANO, DESEMBA 2, 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa akimwita mwanawe 'Majaliwa' patakuwa patamu. Mwanawe ataitwa 'Majaliwa Kassim Majaliwa Majaliwa'

    ReplyDelete

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...