Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Malya akiongea
na mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga wakati
alipotembelea ofisi za Airtel mara baada ya kuwasili kutoka nchini
Marekani alipoenda kurekodi video yake na kupata mafunzo kutoka kwa
mwanamuzi nguli Akon. Safari hii ni moja kati ya zawadi ya kufanya
video na Akon pamoja na mafunzo alizipata mara baada ya kuibuka
mshindi wa shindano hilo Afrika .
 Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Malya
akisalimiana na kumpongeza mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi
Mayunga wakati alipotembelea ofisi za Airtel mara baada ya kuwasili
kutoka nchini Marekani alipoenda kurekodi video yake na kupata mafunzo
kutoka kwa mwanamuzi .
Mayunga akiwa amewasilia uwanja wa ndenge wa julius Kambarage
Nyerere akitokea nchini Marekani.

MSHINDI  wa Airtel Trace Music Stars
Nalimi Mayunga  amerudi nchini kutoka Marekani alipoenda kwa ziara ya
wiki moja kwaajili ya kurekodi video yake na kupata mafunzo kutoka kwa
mwanamuziki nguli Akon

Nalimi Mayunga alisema hii imekuwa nafasi ya pekee maishani mwake  na
anapenda kuwashukuru sana Aitel na Trace kwa kupatia fulsa hii.

“Nimefurahia muda niliokaa mjini Losa Angeles Marekani na kupata
wakati mzuri wa kumtembelea Akon nyumbani kwake na kufanya rekoding ya
video na kupata mafunzo ya musiki alisema.

Nalimi aliongeza kwa kusema fursa hii imenipa mwanga zaidi  katika
namna ya kufikiri na kujipanga ili kuzifikia ndoto zangu katika
tasinia ya muziki.  Nimejifunza mambo mengi sana kupitia mafunzo
niliyopata kutoka kwa Akon ikiwemo jinsi ya kukabili jukwaaa, namna ya
kuchezea sauti yangu, mafunzo ya sauti,  namna ya kuandika na kutunga
nyimbo na jinsi ya kuinua muziki wangu na kukuza kipaji change kwa
ujumla”

Nalimi aliyejawa furaha pia alieeleza shauku aliyonayo ya kutoa kibao
hicho kwa kushirikiana na Akon na kusema kwamba kitafungua milango
yake katika ulimwengu wa muziki kwani amepata nafasi ya kuingia na
kurekodi wimbo wake kwenye studio ya universal Hollywood yenye vifaa
vya kisasa na vyenye technologia ya juu

“ na uhakika video yangu itakuwa moja kati ya video bora za muziki
sokoni na hivyo nawashurukuru sana mashabiki wangu, watanzania  kwa
ujumla kwa kunipigia kura na kuniwezesha kufika hapa nilipo leo”

Akieleza zaidi kuhusu safari ya Mayunga, Mkurugenzi wa mawasiliano wa
Airtel Bi Beatrice Singano Malya alisema “  tunafurahi kuwa sehemu ya
kubadilisha maisha ya vijana wengi akiwemo Nalimi Mayunga. Tunaamini
mayunga atakuwa ni mfano utakaowavutia vijana wengi kuzifikia ndoto
zao. Tunapenda kuwahamasisha vijana wengi zaidi kushiriki katika
program zetu nyingi zenye lengo la kuwawezesha kufikia malengo yako
kama vile Airtel Fursa, Airtel Rising Stars, Airtel Trace Music Stars
na nyingine nyingi .

Msimu wa pili wa shindano kubwa la muziki la Afrika  la Airtel Trace
Music Stars mwaka 2016 linategemea kuzinduliwa rasmi mwanzoni mwa
January 2016, tunatoa wito kwa vijana wengi kushiriki pindi shindano
hili litakapotangazwa rasmi. Aliongeza Mallya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...