WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,
WAZEE NA WATOTO
(TAARIFA
KWA UMMA)
Taarifa inatolewa kwa umma
kwamba Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao chake cha
38 kilichofanyika tarehe 27 Januari, 2016 iliazimia kufuta usajili wa Shirika
la African Poor and Patient Organization
(APOPA) kutokana na kukiuka masharti ya Sheria ya NGOs Na. 24 ya mwaka 2002
(kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005).
Kwa taarifa hii, shughuli za
Shirika tajwa zimekoma kuanzia tarehe ya ttangazo la taarifa hii. Wanachama wa
shirika wanaagizwa kusitisha shughuli za shirika na kuzingatia taratibu za
ufungaji wa shughuli za Shirika kama zinavyoainishwa katika katiba ya Shirika
na Kanuni za Sheria ya NGOs, GN.Na.8 ya Mwaka 2015.
M.S.Katemba
MSAJILI
WA NGOs
2
Februari, 2016
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...