Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizungumza na wadau wa Habari,Michezo na sanaa Mkoa wa Mbeya (hawapo pichani)katika ukumbi wa Mikutano wa Mkapa jijini Mbeya April 2 ,2015 .(Picha Keneth Ngelesi)

Wadau wa Habari,Michezo na Sanaa Mkoani Mbeya wakimsikiliza kwa makini Waziri  wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye wakati wakati akizungumza nao katika ukumbi wa Mikutano wa Mkapa jijini Mbeya.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye (kushoto) akipokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazo husu michezo,sanaa ,burudani kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala katika mkutano maalumu uliowakutanisha ,wadau wa michezo ,sanaa na burudani Mkoa wa mbeya pamoja na baadhi ya viongozi wa halmashauri za mkoa wa Mbeya na Songwe.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akimkabidhi Ipadi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala kwa ajili ya Maafisa Habari wa Mkoa wa Mbeya na Songwe katika kikao maalumu kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa Habari,sanaa,Michezo,kilichoitishwa na Waziri huyo kwa lengo la kujadili changamoto na mafanikio ya  sekta hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Galawa akizungumza katika mkutano huo.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye amesema uamuzi wa serikali kuzuia matangazo  TBC kutokurusha mojakwamoja(live) matangazo ya Bunge ilikuwa na lengo la   kulinusuru shirika hilo lisife kwani lilikuwa likitumia fedha nyingi kwa ajili ya matangazo hayo.
Amesema uamuzi huo ni mkakati wa kuliwezesha shirika hilo kuweza kujiendesha kwani awali lilikuwa likitumia fedha nyingi kwa urushaji wa matangazo ya bunge bila ya malipo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, amesema hayo jijini Mbeya, wakati akizungumza na wadau wa habari,michezo, utamaduni na watendaji wa serikali Mkoa wa Mbeya na Songwe.
Amesema Shirika la utangazaji TBC, lilikuwa linaagizwa kurusha matangazo ya bunge bila ya malipo ambapo kwa mwaka shirika lilikuwa likitumia Bilioni 4 kwa mapato yake ya ndani na kulifanya kushindwa kukarabati mitambo pamoja na mslahi ya watumishi hivyo hivyo uamuzi huo ulikuwa sahihi licha ya wengi kuonesha kutolidhishwa nao.
Amesisitiza kuwa suala hilo litaleta heshima ya Bunge kwani ilifika wakati, baadhi ya wabunge walikuwa wakitoa lugha za maudhi pamoja na kucheza sarakasi mambo ambayo yalikuwa yakivunja heshima ya bunge.
Amesema kutokana na hatua hiyo  Bunge lenyewe ndio limechukua dhamana ya kuanzisha Studio yake  hivyo kutoa fursa kwa Televisheni nyingine kurusha matangazo ya moja kwa moja lakini kulingana na vigezo na masharti yatakayohalalishwa na mamlaka hiyo husika.
Akizungumzia sheria ya baraza la michezo ambayo imekuwa ikilitaja suala la michezo ni hiari na si uchumi, Nape amesema kwa sasa serikali ipo katika mchakato wa kuirasimisha sheria hiyo ili iendane na sera ya michezo ambayo imeweka wazi kwamba michezo kuwa shughuli rasmi ya kiuchumi.
ambapo katika kikao hicho wajumbe walipata nafasi ya kuwasilisha kero na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.
Aidha, akijibu risala iliyotolewa na Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya, ambayo ilimuomba kiongozi huyo kuhakikisha anausimamia mswada huo wa habari katika kulinda maslahi ya wafanyakazi,Nape, aliwataka waandishi wa habari kutambua kuwa maslahi yao wanayoyapigania kutoka kwa waajiri wao, yanajibiwa kwenye mswaada wa sheria ya huduma wa vyombo vya habari.
Alisema, wakati ule ulikuwa ni mwishoni mwa Bunge lililopita hivyo kwa sheria na kanuni za Bunge mswaada huo unatakiwa ukasomwe tena kwa mara ya kwanza, kwa hiyo umefikia pahala pazuri, na kuhakikisha kwamba  maslahi ya waandishi wa habari mule ndani yamelindwa.
Pia, Waziri huyo, aliongeza kuwa serikali inaangalia utaratibu wa kuvifuta baadhi ya  vyuo vinavyotoa elimu ya habari ambavyo havina sifa, kwani vimekuwa vikitoa waandishi wa habari amaboa hawana sifa na kazi yao imekuwa ni kuupotosha umma.
Imeandaliwa na Mtandao wa Kijamii wa 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...