Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO.
JUMLA ya wahalifu 71 wamekamatwa ndani ya siku 7 katika maeneo mbalimbali katika Kata ya Gongo la mboto,Wilaya ya Ilala, Jijini Dar es Salaam wakiwa na kete za bangi pamoja na madumu ya pombe aina ya  gongo.

Idadi hiyo imetajwa leo Jijini Dar es salaam na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi, Bw. Lucas Mkongya alipokua akifafanua juu ya malalamiko ya wananchi wa Gongo la Mboto kuhusu uhalifu uliokithiri katika  maeneo hayo pamoja na jitihada wanazozichukua katika kuzuia uhalifu huo.

“Kweli uhalifu upo na kila siku tunajitahidi kufuatilia maeneo yote ya Gongo la Mboto. ndani ya  siku saba kuanzia Aprili 14 hadi 20 mwaka huu tumekamata jumla ya kete za bangi 640 pamoja na lita 90 za pombe aina ya gongo”alisema Kamishna Msaidizi Mkongya.

Kamishna Msaidizi Mkongya amesisitiza wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu pia amewaomba wananchi wajitahidi  kuunda ulinzi shirikishi utakaosaidia kulinda maeneo yao  kwa sababu polisi pekee  hawawezi kulinda kila nyumba.
Aidha, Kamishna Msaidizi Mkongya ametoa rai kwa wazazi kutoa malezi mazuri kwa watoto wao kwa kuwa asilimia kubwa ya wezi wa maeneo hayo ni watoto wao wenyewe.

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na walinzi shirikishi wanajitahidi kufanya doria kila siku katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam ili kuhakikisha wahalifu wote wanakamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Heri MusokwaApril 21, 2016

    kwa kusema ukweli mimi ni mkazi wa Moshi Bar kwa Diwani kuna eneo linajulikana kwa jina maharufu kwa diwani songosongo kwa Mbowe kuna kilabu cha pombe za moshi( gongo ) na nyingine kwa ujumla wanaita kilabu cha pombe chafu kwa siku za hivi karibuni kumebadilika kuwa sehemu ya kujificha waharifu na gongo inanywewa hadharani na bangi inavutwa kama sigara bila kificho tunaumia sana wakazi wa eneo hilo na hauwezi kulea watoto katika hali hii ukategemea kushinda na mbaya zaidi wakati tunajenga hakukuwa na tabia hizi zimeletwa na watu wanakimbia maeneo mbalimbali kuja kufanya uhalifu hapa tunaomba jeshi la polisi kutusaidia na hata kuwapa ushirikiano tuko tayari kuna wauza Gongo maharufu hapo na jina lingine wanaita machupi bar tafadhali tunawaomba ushirikiano wa jambo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...