Asalaam Aleikhum,
 Awali ya yote nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehma zote.

Ni wiki mbili kamili zitakazotimia leo majira ya saa nane usiku. Muda huo bila shaka nitakuwa katika  anga la dunia nikisafiri kuelekea New Delhi nchini  India kupitia Muscat Oman kwa ajili ya matibabu yangu ya macho.

Usiku wa siku kama ya leo (yaani Jumapili ya tarehe 3-7-2016) niliamka usiku kwa ajili ya daku, Ndipo nilipogundua jicho langu la kushoto halioni kabisa na  jicho langu la kulia lina uoni wake ulikuwa mdogo.Ni siku ambayo sitakaa niisahau maishani mwangu.

Najua madaktari mbali mbali wa hapa nchini walifanya kila jitihada za kunusuru macho yangu ila bado ufumbuzi wa tiba yangu bado haujapatikana. Ndio maana naenda kujaribu India.na Insha Allah Mungu atanivua mtihani huu.

Kiukweli hawa madaktari niwashukuru sana kwa jitihada zao.Rafiki yangu na kaka yangu Dkt. Mohammed wa wizara ya afya, Dkt. Mahunda wa Ocean Road, Dkt. Dalla, Dkt. Chibuga na Dkt. Hassan wa CCBRT na pia Dkt. Datoo wa clinic ya pale Shoppers Plaza Miikocheni. Vile vile Madaktari wa Kituruki pale katika hospitali yao ya International eye clinic maeneo ya Moroco pamoja na wauguzi wao.Mungu atawalipa Insha Allah.
Kipekee niwashukuru ndugu na rafiki zangu wa KT shop. Hapo mimi ndio maskani yangu jioni.Hawa ni zaidi ya binadaam. Kisasa tungesema show nzima ya safari wanasimamia wao.Wamefanya jitihada zote na kiukweli bila wao sijui ingekuwaje.Kwa wiki zote mbili wamekimbizana na mimi ugonjwa wangu bila kuchoka.

Pia niishukuru ofisi yangu klabu ya Simba kwa zaidi ya wema walionifanyia.Niwashukuru viongozi wote, Friends of Simba.wanachama na wapenzi wote wa Unyamani kwa kila jambo na dua zao walizonifanyia..Kiukweli sijutii kupenda na kufanya kazi Simba.

Niishukuru pia serikali ya nchi hii. Nimepokea salaam kutoka kwa Waziri wangu wa michezo.Mhe Nape. Salaam toka kwa waziri na naibu waziri wa afya.Mh Ummy  na Dkt. Kigwangallah. Nimepokea pia salam toka kwa rafiki zangu manaibu waziri Mh Mavunde na Dkt. Possi.

Lakini kipekee kwa waziri wangu wa mambo ya ndani ya nchi. mtani wangu Mh Mwigulu Nchemba ambae yeye mwenyew alikuja kuniona na kwa niaba ya serikali ameahidi kunisaidia kwa kila hali niweze kupona.
Na kwa hapa nisiache kumshukru mwambata wetu wa afya katika  ubalozi wetu nchini India.Dkt.  Goroka kwa kusaidia kupatikana kwa hospitali India.Pia nimshukuru Profesa Mohamed Janabi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ya hospitali Taifa Muhimbili kwa ushauri wake wa kitaalam (nafurahi kusikia jana amethibitiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo nyeti, homgera sana Prof! Unastahili kabisa) .sambamba na daktari wetu wa Simba.
Sitatenda haki kama sitawashukuru viongozi wakuu wa TFF Rais Jamal Malinzi na katibu mkuu wake Mwesigwa kwa kila jambo walilonifanyia. Kipekee niwashukuru viongozi wa dini. mashekh na maustaadh kwa dua zao kwangu.sambamba na wachungaji ambao walikuja hadi kwangu kuniombea..Asanteni sana  watu wa Mungu.
Nisisahau kuwashukuru watani zangu Yanga kwa mchango wao kwangu... Hususan mropokaji 😃😃 wao Jerry Muro.

Nita-mmiss sana kwa fujo na kebehi zake. Ninamuomba awaandikie TFF kuomba radhi na kisha  yeye naye  ajirekibishe kidogo bana....Nna imani TFF  nao wanaweza kupitia kamati zao wanaweza kuangalia namna sahihi ya kulimaliza hili kwa maslahi ya mpira wa miguu nchini. Muhimu Jerry apime tu kauli zake. Mpira si kashfa wala kebehi za kuudhi..na si uadui hata kidogo.

Mwisho niwashukuru ndugu zangu wa Kariakoo Family Development Foundation (KFDF) chini ya mwenyekiti wetu Mohamed Bhinda. Hawa ni Alfa na Omega kwangu Kuanzia niliokuwa nao vjana wa Al-Ahly hadi KFDF. Pamoja nao watu wangu wa nguvu.whatsapp groups zote ambazo zimeniombea sana na kunifariji katiika kipindi hiki kigumu.sambamba na kuja kunijulia hali.

Nikiwasahau wanahabari nitakuwa wa ajabu..Wamefanya kazi kubwa ya kuwahabarisha na kuwapa maendeleo yangu kila siku kupitia vyombo vyao.

Asanteni sana wote! My family. ndugu zangu. jamaa na marafiki wote.nimejua kwa sasa Haji nna watu na nnamuomba mungu niendelee hivihivi na tabia zangu njema nizilojaaliwa na Manani.Msiache kuniombea kwa kila hatua.kuanzia safari yangu.matibabu na kuiombea familia yangu inayobaki hapa nyumbani.

Nawapenda sana. Mungu awabariki sana.

Haji S.Manara

Safarini India

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Twakutakila kila la kheri kaka, In sh Allah Mola atakusimamia katika safari na matibabu yako na In sh Allah atakupa taffif ya haraka.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 18, 2016

    Mimi binafsi ni mshabiki wako, hasa pale unapofanya uchambuzi wa mashindano ya mchezo wa mpira wa miguu.

    Nenda kaka, Allah akurahisishie kila hatua na urudi home ukiwa Haji yule yule wa zamani (shifaa a.

    "Amin"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...