Msanii nyota nchini wa filamu, Jacob ‘JB’ Steven ni miongoni mwa waigizaji mbalimbali walioshiriki katika igizo la Kumekucha ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuhamasisha vijana kujishughulisha na kilimo kutokana na uhaba wa soko la ajira.

Igizo hilo ambali pia ni mchezo wa redio (radio plays) limeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media For Development International (MFDI) chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (Usaid) ya ushauri wa Taasisi ya chakula na lishe (TFNC), Taasisi ya TAHA, ACDI VOCA – NAFAKA, Land O Lakes, Rudi, Mwanzo Bora, The Rice Council of Tanzania, Technoserve, ANSAF (Non State Action Forum) na taasisi ya AMSHA.

Katika filamu hiyo, JB anatumia jina la Mzee Kidevu ambaye kazi yake kubwa ni kununua mazao kwa wakulima kwa bei ya ukandamizaji na kuwafanya wakulima hao kuendelea kuwa na maisha duni huku yeye akijinufaisha.

Akizungumza katika uzinduzi huo, JB alisema kuwa amefurahi sana kushiriki katika filamu hiyo ambayo inafundisha na kuhamasisha vijana kujihusisha zaidi na masuala ya kilimo na kuacha tabia ya kukimbilia mijini kama suluhisho lao la kutatua matatizo yao. “Nimepanda kushiriki katika filamu na mchezo huu wa redio, umenipa mwanga mkubwa na kupanua wigo wa kazi yangu ya kuigiza, kabla ya kuingia kwenye kuigiza, nilikuwa mnunuzi wa mazao hasa mahindi kule Kibaigwa na kusaga na kuuza unga wa chakula, hii ilikuwa fursa kwangu na nimeipenda, nawashukuru wahusika wote waliofanikisha filamu hii,” alisema JB.

Mkurugenzi wa masuala ya Uchumi wa USAID, Randy Chester alisema kuwa wamefurahi kujihusisha na masuala mbalimbali yaa maendeleo hapa nchini na kuamua kusaidia mradi huo ambao unahusika zaidi maeneo ya vijini. “USAID imejihusisha katika miradi mingi ya maendeleo nchini, kama unajua, zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wanajihusisha na masuala ya kilimo, waahitaji kuendelezwa ili kufikia hatua kubwa ya maendeleo, mchezo wa Kumekucha utawaamsha na kupata maendeleo,” alisema Chester. 
Muigizaji nyota wa filamu nchini, Jacob Steven (JB) akiizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na igizo jipya lilijulikanalo kwa jina la Kumekucha ambalo imeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media For Development International (MFDI) chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (Usaid). Katika igizo hilo, JB ametumia jina la Mzee Kidevu. Muandishi wa ‘script’ ya igizo la Kumekucha, Priscilla Mlay (kulia) akizungumza wakati wa utambulisho wa igizo la Kumekucha ambalo limeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media For Development International (MFDI) chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (Usaid). Mkurugenzi wa masuala ya Uchumi wa USAID, Randy Chester (wa kwanza kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa igizo hilo la Kumekucha utawaamsha na kupata maendeleo,” 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...