Kocha Jose Mourinho hakuamini macho yake alipoishuhudia timu yake ya Manchester United ikipokea kichapo cha mbwa mwizi cha mabao 4-1 toka kwa vijana wa Borussia Dotmund kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliomalizika muda mfupi uliopita huko nchini China.

Alikuwa ni mchezaji Castro katika dakika ya 19 aliyeanza kuwakosesha raha mashabiki wa Manchester baada ya kuandika bao la kwanza kufuatia piga nikupige langoni mwa Manchester. 

Dakika 36 mlinzi Antonio Valencia aliunawa mpira ndani ya kumi na nane na mwamuzi akaamuru Upingwe mkwaju wa penati na mshambulizi hatari wa Dotmund Mkhitaryan Aubemayang akapiga kiufundi penati hiyo na kuandika bao la pili.

Kipindi cha pili dakika ya 57 Dembele akawafungasha tela mabeki wa Manchester na kufunga goli zuri sana na kufanya matokeo kuwa goli 3-0. Manchester walijitahidi kufurukuta na kujipatia goli la kufutia machozi lililofungwa na Malta.
Dakika za mwishoni wa mchezo Castro aliyekuwa mwiba mkali kwa mabeki wa Man U alidhihirisha ubora wake pale alipofunga bao la nne na kumfanya kocha Jose Mourinho aduae nafikiri akidhani yumo ndotoni.Wachezaji wa Man U wanaonyesha bado wanahitaji muda mrefu wa kucheza kitimu kwani hawakuwa na muunganiko mzuri wa kitimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...