Wananchi wa kijiji cha Kurutu kilichopo kata ya Shungubweni wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani wameshauliwa kuchukua shamba lenye ukubwa wa hekari 66.6 ambalo alipewa mwekezaji tangu mwaka 1988 na kushindwa kuliendeleza,ili walitumie Kwa shughuli za kuzalisha mali.

   Ushauri huo ulitolewa wilayani humo na Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Abdallah Ulega mara baada ya kupokea malalamiko kutoka Kwa wananchi wake  akiwa katika ziara zake za kushukuru wanakijiji hao Kwa kumchagua kuwa mbunge wao.

Ulega alisema haiwezikani watu wanajimilikisha mashamba makubwa miaka hadi miaka alafu wanashindwa kuyaendeleza huku wananchi wakipata shida ya kukosa maeneo hata ya kulima kilimo cha mbogamboga vijana.

 "Nasema kuwa kama shamba hilo limekaa miaka yote hiyo haliendelezwi, na pia huyo mwekezaji haonekani sasa mnasubiri nini kulichukua na kufanya uendelezaji. Nashauri litwaeni halafu tutapambana naye huko mbele"

Pia Ulega aliwaeleza wananchi hao kuwa siasa imekwisha na kilichobaki ni watu kufanya Kazi Kwa nguvu zote na kwamba  atakuwa bega Kwa bega  katika kuhakikisha maendeleo  wanayapata Kwa haraka.

Awali wananchi  wa kijiji cha Kurutu walimweleza mbunge kuwa wanavshamba kubwa ambalo alipewa mwekezaji miaka mingi iliyopita tena kienyeji lakini hadi leo ameshindwa kuliendeleza hivyo awasaidie walipate ili vijana wa eneo hilo wazalishe chumvi.

 Mbunge huyo bado anaendelea na ziara zake za kutembelea kijiji hadi kijiji kwa lengo la kuwashukuru na kuhimiza shughuli za maendeleo ambapo anawataka kujituma katika kufanya kazi kwani wilaya hiyo imechelewa kimaendeleo.
 Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mhe Abdallah Ulega akielekea kijiji cha Kurutu kilichopo kata ya Shungubweni wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani kwa mtumbwi.
 Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega akikagua daraja
 Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na walimu wa shule ya  msingi  ya kijiji cha Kurutu kilichopo kata ya Shungubweni 
 Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na  wananchi wa kijiji cha Kurutu kilichopo kata shungubweni wilayani Mkuranga katika ziara zake za kushukuru wanakijiji hao Kwa kumchagua kuwa mbunge wao.
Mwanakijiji Shabani Omary  akiuliza swali kwa mbunge wa jimbo la mkuranga Mhe. Abdallah Ulega. Habari na picha na Emmanuel Masaka wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. mbunge inabidi utijahidi kubuni njia za kunyanyua vipato vya wananchi wako kwani wanaoekana kuchoka kimaisha. hilo daraja linatia aibu fanya mchakato hela za jimbo zijenge darala la kueleweka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...