Kulia Meneja wa Airtel Money Bw, Asupya Nalingigwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi Mr Money wa Airtel Money atakavyogawa faida ya shilingi billion 3 kwa wateja wa Airtel Money na mawakala wake nchi nzima ikiwa ni faida yao kutokana na kutumia Airtel Money kuanzia Januari hadi juni mwaka huu kushoto ni Meneja wa uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando jana.
 Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa kugawa gawio la faida ya shilingi billion 3 kwa wateja wa Airtel Money na mawakala wake nchi nzima ikiwa ni faida yao kutokana na kutumia Airtel Money kuanzia Januari hadi juni mwaka huu. Kulia ni Meneja wa Airtel Money Bw, Asupya Nalingigwa jana.


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa gawio la faida la kila kiasi cha shilingi billion 3 kwa wateja wake wa Airtel Money na mawakala wakubwa na wadogo nchi nzima

Airtel imetoa gawio la faida kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi juni mwaka huu ambapo kila mteja atalipwa sehemu ya faida kulingana na kiasi cha salio lake katika akaunti yake ya Airtel Money kila siku

Akiongea na waandishi wa habari , Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando alisema “Tunayofuraha kutoa gawio la faida la shilingi bilioni 3 kwa wateja wetu na wakala nchi nzima. Tunaamini gawio hili la faida litawawezesha wateja wetu kutatua mahitaji yao ya kifedha na hivyo kuthibitisha dhamira yetu ya kuendelea kutoa huduma za kifedha”

“Tumejipanga kuwawezesha wateja wetu kwa kupitia huduma na bidhaa tunazozitoa. huduma ya Airtel Money imelenga kuleta unafuu na kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha katika maeneo mbalimbali nchini hususani ya maeneo ya pembezo mwa nchi. Aliongeza Mmbando

Mpaka sasa Airtel imeshatoa kiasi cha shilingi billion 10 kwa wateja na mawakala wa Airtel money tangu  2014.

Huduma ya Airtel Money inawawezesha wateja kufanya miamala mbalimbali ikiwemo kutuma na kupokea pesa, kulipia bili, kununua vifurushi, kuamisha pesa na kutoa pesa kutoka benki pamoja na kutoa mikopo isiyo na dhamana kupitia huduma ya Airtel Timiza ambayo inatoa mikopo ya haraka, rahisi kwa wateja na mawakala.


Mpaka sasa mtandao wa mawakala 50,000 wa Airtel Money nchini Tanzania wanaweza kutumia huduma hii. Theluthi moja ya mawakala wote wa Airtel Money hutumia Timiza, na baadhi ya mawakala sasa hivi wanakidhi vigezo vya kupata mikopo hadi Shilingi milioni moja. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...