Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa kijamii wa Airtel FURSA ikishirikiana na Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) imeendelea kuwawezesha vijana kupata kozi mbalimbali zinazotolewa katika vituo vya VETA nchini kupitia application ijulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO.

Akiongea na waandishi habari afisa Uhusiano wa Airtel Dangio Kaniki alisema, “vijana wameufurahia sana mpango huu unaowawezesha kusoma masomo kutoka VETA kwa urahisi zaidi na kuchochea kukua kwa elimu kwa vijana wengi na kuwawezesha kupata ujuzi wa ufundi na biashara itakayoongeza ufanisi wao”.

“Mafunzo kwa njia ya mtandao ni rahisi na yatapatikana kwa wateja wa Airtel wenye simu zenye mfumo wa android. Mteja atatakiwa kupakua application ya VSOMO kwenye orodha ya menu yake ya simu sehemu ya google play store na kujiandikisha bure. 
Mara baada ya kumaliza masomo yake kwa 40% mwanafunzi atatakiwa kwenda kwenye kituo cha VETA kilichopo karibu nae na kujiandikisha kwaajili ya mafunzo kwa vitendo ambayo yatachukua muda wa wiki 2 kumaliza ikiwa ni sawa na masaa 60 na ndipo atakapokaa kwaajili ya mtihani na kutakiwa kufaulu kwa 60% “alisisitiza Kaniki

Aliendelea kusema kuwa “vijana zaidi ya 19000 wamejisajili kusoma kozi mbalimbali kutoka VETA kupitia simu zao za mkononi. Kwasasa masomo yanayopatikana ni Ufundi pikipiki (bodaboda), Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium, utaalamu wa maswala ya urembo na ufundi wa kuchomelea vyuma.”

Akibainisha hayo Kijana Saleh Shomari anayesoma kozi ya ufundi umeme kupitia application ya VSOMO alisema “ VSOMO imekuwa msaada kwangu maana nilikuwa natamani kusoma kozi VETA lakini sikuwa na mda wa kufika chuo cha VETA kutokana na mihangaiko ya biashara zangu, lakini nawashukuru Airtel na VETA kulionahili na sasa najisomea mafunzo haya ya umeme jioni nikishafunga biashara yangu na kuweza kufikia malendo yangu ya kupata cheti kutoka VETA.”

Dangio alimalizia akisema” Mwanafunzi atatahiniwa na kisha kuandikishwa na kutakiwa kulipia kiasi shilingi 120,000/= kwa kupitia Airtel Money kwa kupiga *150*60# kama gharama ya mafunzo hayo. Tunatoa wito kwa vijana kutumia fursa hii ya kipekee ili kupata mafunzo ya ufundi kwa urahisi na gharama nafuu kwani gharama ya masomo iko chini zaidi.”

Afisa Uhusiano na matukio wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mafanikio ya mafunzo ya stadi za ufundi yanayotolewa na VETA kupitia mtandao wa simu ya mkononi wa Airtel yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO katika ofisi za makao makuu ya Airtel Tanzania zilizoko Moroco jijini Dar es Saalam hapo jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...