THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

AIRTEL NA VETA KUENDELEA KUELIMISHA VIJANA KUPITIA VSOMO APPLICATION

 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa kijamii wa Airtel FURSA ikishirikiana na  Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) imeendelea kuwawezesha vijana kupata kozi mbalimbali zinazotolewa katika vituo vya VETA nchini kupitia application ijulikanayo kama “VSOMO”  yaani VETA SOMO. 
Akiongea na waandishi habari afisa Uhusiano wa Airtel Dangio Kaniki alisema, “vijana wameufurahia sana mpango huu unaowawezesha kusoma masomo kutoka VETA kwa urahisi zaidi na kuchochea kukua kwa elimu kwa vijana wengi na kuwawezesha kupata ujuzi wa ufundi na biashara itakayoongeza ufanisi wao”. 
“Mafunzo kwa njia ya mtandao ni rahisi  na yatapatikana kwa wateja wa Airtel wenye simu zenye mfumo wa android.  Mteja atatakiwa kupakua application ya VSOMO kwenye orodha ya menu yake ya simu sehemu ya google play store na kujiandikisha bure.  Mara baada ya kumaliza masomo yake kwa 40% mwanafunzi atatakiwa kwenda kwenye kituo cha VETA kilichopo karibu nae na kujiandikisha kwaajili ya mafunzo kwa vitendo ambayo yatachukua muda wa wiki 2 kumaliza ikiwa ni sawa na masaa 60  na ndipo atakapokaa kwaajili ya mtihani na kutakiwa kufaulu kwa 60% “alisisitiza Kaniki. 
Aliendelea kusema kuwa “vijana zaidi ya 19000 wamejisajili kusoma kozi mbalimbali kutoka VETA kupitia simu zao za mkononi. Kwasasa masomo yanayopatikana ni Ufundi pikipiki (bodaboda), Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium, utaalamu wa maswala ya urembo na ufundi wa kuchomelea vyuma.” 
Dangio alimalizia akisema” Mwanafunzi atatahiniwa na kisha kuandikishwa na kutakiwa kulipia kiasi shilingi 120,000/= kwa kupitia Airtel Money kwa kupiga *150*60# kama gharama ya mafunzo hayo. Tunatoa wito kwa vijana kutumia fursa hii ya kipekee ili kupata mafunzo ya ufundi kwa urahisi na gharama nafuu kwani gharama ya masomo iko chini zaidi.”