Msanii, Ally Salehe 'Ali Kiba' akishambulia jukwaa wakati akitumbuiza kwenye  tamasha la kutimiza miaka Miwili ya Chaneli ya Startimes Swahili tokea kuanzishwa Kwake. Tamasha hilo lililopewa jina la Serebuka Festival lililofanyika katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jana ambapo lilidhaminiwa na Kampuni ya Huawei Tanzania.
 Msanii, Snura Mushi, akitumbuiza kwenye tamasha hilo.
 Msanii, Juma Kassim 'Juma Nature, akitumbuiza kwenye 
tamasha hilo.
 Msanii Stamina akipagawisha  kwenye tamasha hilo.
Wananchi wakifuatilia Tamasha la Serebula Festival la kuazimisha miaka miwili ya chanel ya startimes Swahili iliyoandaliwa na kampuni ya Bluelines kwa kushirikiana na uwawei jijini Dare s Salaam jana.
Na Dotto Mwaibale
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Judith Wambura Lady Jay Dee na Ali Salehe Ali Kiba wameonesha umahiri wao wa kuimba kwa kutumia 'live band' katika tamasha la Serebuka na Festival 2016 lililofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mashabiki walioudhuria tamashan hilo walianza kuonesha shangwe baada ya Lady Jay Dee kupanda jukaani na kuimba tungo na alioimba wimbo wa Ndindindi mashabiki walilipuka kwa vifijo.
Shangwe hizo zilidumu hata kwa msanii Ali Kiba ambapo walimtaka aendelee kuimba licha ya muda wa kuendelea na tamasha hilo kuwa umekwisha.
Ali Kiba aliwachangua zaidia mashabiki walipoimba wimbo wa Aje ambpo dakika za mwisho jukwaani hapo akapanda mwanadada na kushuka na msanii huyo na kuacha mashabiki wakishangilia kwa shangwe.
Wasanii wengine ambao walionesha uhai katika tamasha hilo, Bonivecture Kabobo 'Stamina' ambaye mashabiki walionesha kumuunga mkoano kutokana na aina ya uimbaji wake kuteka mashabiki.


Pia katika tamasha hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya King'amuzi cha Starv Times liliudhuriwa ma Juma Kasimu 'Juma Nature', Madee,Yamoto Band, Snura  na wengineo ambao waliimba kwa kutumia 'Play Back'.
Tamasha hilo lililopewa jina la Serebuka Festival liliandaliwa  na Kampuni ya StarTimes na  Kudhaminiwa na Kampuni ya Huawei Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. The mdudu, hahaha haaaaa mbona habari yenyewe imekaa kwa kuegamia pande mbili tuuuu? why eti Lady Jay Dee na Ali Kiba ndio walio funika ila wengine walionyosha uhai sasa kama mwandishi kweli una fuatilia mambo ya music hivi kweli mtu kama Ali Kiba unaweza kum fananisha na Juma Nature au hao watoto Yamoto Band? achilia huyo mkali wao Stamina toka kule Moro ndugu zangu wanahabari tuwe tuna watendea haki, ukweli usio fichika wanamusic wetu kwenye upande wa kuimba live ni bado sana tena sana hapa nawa zungumzia wa music wa kizazi kipiya coz wao hawaendani kabisa na vyombo kelele mtindo mmoja yaani wanapooza sana jukwaani hasa hasa huyo Ali Kiba ndio kabisaaa ila ukitaka kui njoy music wa live ni bora uende kwa Msondo Ngoma na Skinde Ngoma ya ukae mjomba Michuzi please nifikishie huu ujumbe mimi nimezaliwa kusema ukweli siku zote msema ukweli ni mpenzi wa Mungu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...