THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

ATOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA

MKAZI wa kijiji cha Kabare kata ya Uwarama wilaya ya Kakonke, Robent Laurent (35) ametoweka nyumbani kwake Dodoma Makulu katika mazingira ya kutatanisha.
Kwa mujibu wa Shemeji yake, Mchungaji Philip Kayanda, amesema kuwa Laurent alikuwa ametokea Zanzibar na kuelekea Kahama lakini alipofika hapa Dodoma aliteremka na kuelekea nyumbani kwao eneo la Dodoma makulu ambako alitoweka kusikojulikana. Pia  alisema kuwa shemeji yake huyo ana matatizo ya akili.
Laurent ambaye rangi yake ni maji ya kunde amesema kabla ya kujachanganyikiwa akili, alikuwa anafanya kazi ya uchungaji katika kanisa la FPCT huko kijijini kwao Kabare mkoa wa Kigoma ikiwemo na Zanzibar.

Amesema jitihada za kumtafuta kwa ndugu, jamaa na marafiki zimefanyika bila mafanikio na tayari wametoa taarifa kituo cha polisi kati cha Dodoma na kufungua jalada namba RB/DOM/8409/2016.
Ameomba kwa yeyote atakayemuona atoe taarifa katika kituo chochote cha polisi kilichopo karibu ama apige simu namba 0688 - 688229,0788 – 669300 au 0655 – 090820