Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  anayesimamia sekta Mawasiliano mhandisi Dkt. Maria Sasabo kushoto akizungumza wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa vyuo, sekondari na shule za msingi za jijini Dar es Salaam walioshinda shindano la uandishi wa insha kuhusu haki ya mtumiaji wa huduma za mawasiliano, kulia ni Katibu wa Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano  Bi. Mary Shao Msuya.

 Mwenyekiti wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano Bw. Stanley Mwabulambo akimkaribisha mgeni rasmi  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Mawasiliano) Mhandisi Dkt. Maria Sasabo kuzungumza na wanafunzi wa vyuo, sekondari na shule za msingi za jijini Dar es Salaam walioshinda shindano la uandishi wa insha kuhusu haki ya mtumiaji wa huduma za mawasiliano 

 Mshindi wa kwanza wa insha kwa upande wa Shule za Msingi  Jane Michael Andrew  kutoka shule ya msingi ya Mbuyuni akipokea zawadi ya cheti ya mshindi wa kwanza wa insha kutoka kwa Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Mawasiliano) mhandisi Dkt. Maria Sasabo.
 Mshindi wa kwanza wa insha kwa upande wa vyuo vya elimu ya juu Bw. Omari Abbas kutoka chuo Kikuu kishiriki cha Ualimu (DUCE) akipokea zawadi ya cheti kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Mawasiliano) mhandisi Dkt.   Maria Sasabo.
Mshindi wa kwanza wa insha kwa upande wa Shule za sekondari Bw, Ramadhani Mohamed kutoka Shule ya sekondari ya Kibasila  akipokea zawadi ya mshindi wa kwanza wa insha kutoka kwa Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Mawasiliano) mhandisi Dkt. Maria Sasabo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...