Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Msanii wa muziki wa taarab Bi. Shakila Said kilichotokea ghafla nyumbani kwao Mbagala jijini Dar es Salaam jana Ijumaa ya tarehe 19/08/2016.

Shakila ni msanii na mdau wa muda mrefu wa sekta ya Sanaa nchini. Amekuwa na mchango mkubwa katika kukuza muziki wa taarab nchini hasa katika kubuni kazi za Sanaa za muziki mbalimbali ambazo zilikuja kupata umaarufu mkubwa. Moja ya kazi alizobuni na kupata umaarufu mkubwa ni pamoja na 'Macho yanacheka' na 'kifo cha mahaba'.

Mchango wake katika muziki wa taarab hasa katika kubuni na kutunga nyimbo zenye ubora, ujumbe na maadili kwa jamii hautasahaulika kamwe. Ni mwanamuziki aliyeacha misingi katika sekta ya muziki na alijitolea kwa kiasi kikubwa katika kuufikisha muziki wa taarab mahali ulipo leo.

Baraza, wasanii na wadau wote wa Sanaa hatuna budi kuendelea kuenzi mema yote aliyotuachia marehemu Shakila hasa katika kupenda kujitolea muda mwingi katika kukuza muziki wa taarab na sekta ya muziki kwa ujumla.

Baraza linatoa pole kwa ndugu wa marehemu, shirikisho la muziki, wasanii na wadau wote wa Sanaa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hakika Bi Shakila Said Hamis amekuwa ni mchango mkubwa kwa Taifa hili tangu 1961 hadi kufikia umauti wake, amekuwa mstari wa mbele na muasisi wa muziki huu wa Taarab hadi leo kufikia hapa ulipo. Kwa kweli ni pigo na pengo kubwa kwa Taifa khususan katika fani hii ya muziki wa Taarab na khasa kwa wale wapenzi wake wote wa Taarab Asilia ndani na nje ya nchi. Mola mlaze pema peponi Amen. Yeye katangulia nasi sote umauti ndio khatamia yetu na kwa Mola tutarejea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...