THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Benki ya CRDB imekanusha vikali habari kwamba imesimamisha mikopo kutokana na "hali tete ya uchumi wa nchi ".

Benki ya CRDB  imekanusha vikali habari iliyoandikwa leo Agosti 18, 2016 na  gazeti moja la kiswahili la kila siku na kunukuliwa na baadhi ya mitandao ya kijamii na  kumnukuu kimakosa Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Charles Kimei (pichani) kuwa Benki hiyo  “Sasa imesimamisha mikopo kutokana na "hali tete ya uchumi wa nchi ".

Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB Bi. Tully Esther Mwambapa, amekanusha  vikali habari hiyo ambayo ameitaja kuwa  inalenga kuwatia hofu wateja wao  wapendwa na kuichonganisha Benki ya CRDB na dola.

“Nachukua fursa hii kuwatangazia wateja wetu na watanzania wote kwa ujumla kuwa waipuuze taarifa hii na kuwajulisha kuwa Benki inatoa mikopo kama kawaida na tunawakaribisha kuja kukopa ili kwa pamoja tujenge uchumi wa taifa letu”, amesema Bi. Mwambapa katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo.