Viongozi wa Timu ya Kagera Sugar, Wanamkurukumbi wakiteta jambo leo kwenye Uwanja wa Kaitaba kwa mara ya kwanza Tangu Uwanja huo ukamilike hivi karibuni. Na sasa ukiwa tayari kwa Michezo mbalimbali ikiwemo Mitanange ya Ligi Kuu Vodacom. Kagera Sugar wanajifua kujiandaa kwa Mchezo wao wa tarehe 3 Septemba, 2016 dhidi ya Mwadui kutoka Shinyanga ambapo nmchezo huo utapigwa katika Uwanja huo ambao umejengwa tayari kwa Viwango vya Fifa. ‘Wanankurukumbi’ walipambana hadi siku ya mwisho kukwepa mkasi wa kushuka daraja msimu uliopita wakiwa na kocha wao Adolf Rishard na sasa wakiwa na Kocha mpya msimu huu mpya 2016/2017 Mecky Mexime ambao pia wamefanya usajili wakiwemo makipa. Leo wameanza kujifua kwenye Uwanja wao kwa ajili ya kuhakikisha hawakumbwi na gharika iliyowakosa msimu uliopita na hatimae kufanya vyema kwa msimu huu ambao umeanza kwa aina yake wakianzia ugenini mechi zao mbili za mwanzo.
Wakiomba kabla ya kufanya Mazoezi leo hii jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Mwenyekiti wa kamati ya Waamuzi ya TFF, Salum Umande Chama ambaye pia ni Katibu wa KRFA (katikati) kulia ni Makamu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), WALLACE KARIA nao walikuwepo Uwanjani hapo kujionea Uwanja huo ambao umemalizika kwa kusuasua. 
Mecky Meximeakitoa maelekezo kwa wachezaji wake leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba, Wakijiandaa kuikaribisha Timu ya Mwadui hivi karibuni.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwa jinsi serikali hii inataka ni vizuri kujitolea...naombeni kabla ya mazoezi yajayo waamasishe mashabiki wenu jumamosi asubuhi kila mtu na koleo jembe na fyekeo mkafyeke nyasi ninazoziona majukwaani..infact mi niko dar ningekuwa home ningekuwa wa kwanza...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...