Timu ya wavulana ya Blue Star jana wametangazwa mabingwa wa vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars baada ya kuwafunga timu ya Makongo Sekondari 2-0 kwenye mchezo uliokuwa wakuvutia uliochezwa jana kwenye uwanja wa Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.
Kwenye mchezo huo ambao ulivuta umati mkubwa wa mashabiki, ulitanguliwa na mchezo wa fainali wa wasichana kati ya Mburahati Queens na Upendo Queens ambapo Mburahati Queens waliibuka na ushindi wa 1-0, huku Fatuma Idd akiifungia timu yake bao pekee kwenye dakika ya 46 ya mchezo.
Kwenye mechi ya wavulana ambayo Makongo walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda lakini walijikuta wakishindwa kufurukuta mbele ya Blue Stars ambayo washambuliaji wake walikuwa wakilishambulia lango la wapinzani wao mfululizo.
Timu ya Blue Star walijipatia bao lakuongoza dakika ya 20 kupitia kwa Shabani Mangula kwa mpira wa kichwa, akimalizia kazi nzuri iliyoanzia upande wa kulia. Baada ya bao hilo, Makongo waliongeza mashambulizi kutafuta goli la kuzawazisha, lakini juhudi zao zilikuwa zikiishia kwa mabeki wa Blue Stars ambao walicheza kwa umakini mkubwa muda wote wa mchezo.
Hadi kipindi kwa kwanza kinamalizika, Blue Star walikuwa mbele kwa bao moja. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana huku Makongo wakitafuta goli la kusawazisha lakini walijikuta kwenye hali ngumu zaidi baada ya mshambuliaji wa Blue Star Ally Hamisi Ally kuifungia timu yake goli la pili dakika ya 47
Goli hilo liliamsha nderemo kutoka kwa mashabiki wa Blue Star ambao walikuwa wamejitokeza kwa wingi kushangilia timu yao.
Wakati Mkoa wa kisoka wa Kinondoni wakifikia tamati ya michuano ya Airtel Rising Stars 2016, mechi zingine za michuano hiyo zilikuwa zikiendelea katika mikoa ya Mbeya, Temeke, Mwanza na Zanzibar jana. Timu ya Mbagala ya Temeke walizindisha ndoto za kushinda taji kwa mkoa huo baada ya kushinda 1-0 dhidi ya Twalipo kwenye uwanja wa Tandika Mabatini.
Mkoani Mwanza, Timu ya Hamasa FC waliwafunga Nyamangana United 2-1 kwenye nusu fainali ya kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa DIT.
Mechi za mkoa zitafuatiwa na fainali za taifa za michuano ya Airtel Rising Stars ambazo zitafanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam Septemba 6 mpaka 11.
 Mchezaji Israel Luvamba wa timu ya Blue Star na Salum Mkana wa Makongo Sekondari wakigombania mpira wakati wa fainali za Airtel Rising Stars mkoa wa Kinondoni. Blue Star walishinda 2-0.
 Nahodha wa timu ya wasichana ya Mburahati Queens Shehati Juma akipokea kombe kutoka kwa Diwani wa Kata ya Vikumbulu Siri Gongo baada kuwafunga Upendo Queens 1-0 kwenye fainali za michuano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Kinondoni. Mchezo huo ulifanyika kwenye uwanja wa Tanganyika Packers.
Timu ya Mburahati Queens wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe kuwa washindi wa michuano ya Airtel Rising Stars (wanawake). Mburahati waliwafunga Upendo Queens 1-0 kwenye uwanja wa Tanganyika Packers, Dar es Salaam.

Nahodha wa timu ya Blue Star Ally Hamisi Ally akipokea kombe kutoka kwa Katibu wa Chama cha Mpira wa Wanawake mkoa wa Dar es Salaam Stephania Kabumba kwenye uwanja wa Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam jana. Blue Star walishinda 2-0 dhidi ya Makongo Sekondari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...